Manusura wa Ajali ya Ndege Iliyopinduka Miguu Juu, Kupewa Milioni 77 Kila Mmoja
Shirika la Ndege la Delta la Nchini Marekani, limesema litawapatia Abiria walionusurika kwenye ajali ya moja ya Ndege zake Nchini Canada kiasi cha dola za kimarekani 30,000 kila mmoja (takriban shilingi 77.8 milioni) kama msaada usio na masharti.
Ndege hiyo namba 4819 iliyokuwa imebeba Watu 80, iliyokuwa ikitoka Minneapolis ilipata ajali na kubinuka juu chini wakati wa kutua mjini Toronto siku ya Jumatatu na kusababisha Watu kadhaa kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa Delta kati ya Abiria 21 waliowahishwa hospitalini, 20 walikuwa tayari wameruhusiwa kufikia siku ya Jumatano asubuhi.
Msemaji wa Kampuni hiyo amesisitiza kuwa malipo haya ya dola elfu 30 kwa kila mmoja hayana masharti yoyote na hayatoathiri haki za Abiria hao ambapo pia Timu yake ya msaada wa dharura ya Shirika hilo inaendelea kuwahudumia Abiria hao katika kipindi hiki cha baada ya ajali ikihakikisha wanapata msaada wanaohitaji.
ليست هناك تعليقات