Subscribe Us

Breaking News

UBAYA UBWELA WAKUTANA NA NAMUNGO, YAPIGWA 0-3 SIMBA


LEONEL Ateba anasalia na mabao 8 ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya kukosa penalti dakika ya 51 mbele ya Namungo baada ya kipa Jonathan Nahimana kuokoa penalti hiyo iliyosababishwa na Elie Mpanzu.

Ubayaubwela umeibukia Namungo kwa pointi tatu kuwa mali ya Simba wakiwa ugenini ndani ya dakika 90 kwenye mchezo wa mzunguko wa pili.

Namungo wanakwama kukomba pointi mbele ya Simba msimu wa 2024/25 mchezo wa mzunguko wa kwanza walipoteza mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.

Ni pointi tatu Simba imekomba mbele ya Namungo kwa ubao wa Uwanja wa Majaliwa kusoma Namungo 0-3 Simba huku Shomari Kapombe akisababisha penalti mbili.

Kiungo Jean Ahoua katupia mabao mawili yote kwa penalti dakika ya 45+8 na dakika ya 71 na Steven Mukwala alipachika bao moja dakika ya 90.

Simba ni nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 50 baada ya mechi 19 vinara ni Yanga wenye pointi 52 baada ya kucheza mechi 20.

ليست هناك تعليقات