Subscribe Us

Breaking News

Elly Kinngu: Soka la Tanzania Litaenda Kuanguka Anguko Kubwa Sana

 Elly Kinngu: Soka la Tanzania Litaenda Kuanguka Anguko Kubwa Sana



Ameandika Elly Kinngu:

Watanielewa wenye akili peke yao, Soka la Tanzania si miaka mingi mtaniambia litakwenda kuanguka anguko kubwa sana. Kuna upumbavu mwingi sana unaendelea kwenye ligi hadi unajiuliza hivi tumekosa hata aibu kama nidhamu haipo? Unashangaa makocha wanatoa kauli za kipuuzi kabisa katikati ya mashindano ya ligi, unashangaa team zinachukuliana makocha na kuona wazi kabisa kuna element zote za kupanga matokeo, unashangaa team inaingiza uwanjani team B makusudi ili team fulani ishinde.

Huu upumbavu sisi watu wenye akili zetu tunautukera mbaya zaidi. Bodi ya ligi imelala, TFF wamelala, na kwakua wote mmeshikwa ganzi mimi mtoto wa Mwalimu Kingu (Bwana aendelee kumpa pumziko hadi ajapo tena) nawambia andikeni hapa chini ubora wa ligi hii utaporomoka kwa kasi miaka minne ijayo. Kwa nchi changa ambavyo mpira wake bado haujakuwa, unachora njia moja anafadhili hata kama sio full ugadhili, team inaonewa, kwa mazingira ya Tanzania kila siku matokeo yanatungwa.

Huwezi kuona mafanikio na shida hizi, Nike, Emirates, huwezi mkuta CEO wa Emirates au Nike anapanda bus kwenda kuangalia Pamba inacheza na refa gani anachezesha. Kuweni na kiburi lakini haya mtayavuna very soon. Tunapokosa nidhamu kwenye mambo haya ni wazi tunahujumu nchi na vipaji vya watoto wa taifa hili. Kwa kuwa wamejaa viburi, watasema haka ka mbunge kachochezi. Kuna team zinaumia sana ila ukiangalia zinajituma sana

ليست هناك تعليقات