Hali katika mji wa Goma
Unapotembea katika mji wa Goma, mitaa inavuma kwa pikipiki. Maduka mengi yamefunguliwa, na wauzaji katika magenge wamerudi na marundo yao ya vitunguu, parachichi na nyanya.
Wapiganaji wa M23 wenye silaha hawaonekani. Hawapo kwenye kona za barabara. Hawana haja ya kufanya hivyo. Kila mtu anajua wao ndio wanadhibiti mji.
"Watu wangemkubali shetani hapa, ikiwa wanaamini ataleta amani," anasema mwanaume mmoja.
Wengine wako makini sana. Mwandishi wa habari anasema, vyombo vingi vya habari "vinajidhibiti" juu ya kile wanachoripoti, wakisubiri kutathmini jinsi watawala wapya watakavyokuwa.
Mwanaharakati mmoja amenambia, wengi wa wanaharakati "wanaishi katika ukimya mkubwa" kwa sababu ya kuogopa kulipiziwa kisasi na waasi.
"Hiki ni kipindi cha wasiwasi zaidi katika historia ya Goma," anasema. "Naogopa, siku zijazo hazina uhakika."
ليست هناك تعليقات