Subscribe Us

Breaking News

MABADILIKO MAMLAKA YA MAJISAFI MOROGORO MORUWASA

 

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amefanya mabadiliko katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA).

Waziri Aweso katika mabadiliko hayo amemteua CPA Sais Andongile Kyejo kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA.

CPA Kyejo ni Mkurugenzi wa Fedha wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ambapo anachukua nafasi ya Mhandisi Tamimu Katakweba.

Waziri Aweso amechukua hatua hiyo kwa Mamlaka aliyopewa kupitia Sheria Na. 5 ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira ya Mwaka 2019 Sura 272 pamoja na Sheria ya Kutafsiri Sheria Sura Na. 1.

Pamoja na hayo, amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri kuunda timu maalumu ya Wataalamu kufanyia kazi changamoto ya hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika manispaa ya Morogoro na eneo lote linalohudumiwa na MORUWASA.

ليست هناك تعليقات