
KLABU ya KMC imepoteza mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex baada ya dakika 90 wamepoteza kwa kushuhudia ubao ukisoma KMC 1-6 Yanga.
Kiungo mshambuliaji Aziz Ki ambaye ametupia mabao matatu ilikuwa dakika ya 18 kwa mkwaju wa penalti, dakika ya 49 na dakika ya 56 kwa penalti Prince Dube lingine kwa Yanga ni bao moja alipachika dakika ya 10 lile la sita Israel Mwenda ni dakika ya 90 na lile la KMC limefungwa na Redemtus Mussa dakika ya 51 kwenye mchezo wa leo ambapo kiungo Clatous Chama alianzia benchi.
Pointi tatu ambazo wanazipata Yanga Februari 14 2025 zinawafanya wawe vinara wa ligi namba nne kwa ubora Afrika wakiishusha Simba iliyokuwa nafasi ya kwanza.
Yanga inafikisha pointi 49 ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo inaishusha Simba ambayo inakuwa nafasi ya pili na pointi 47 kibindoni baada ya kucheza mechi 18 na Yanga mchezo wa leo ulikuwa ni wa 19.
Aziz Ki amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo wa leo kutokana na kiwango ambacho amekionyesha ukiwa ni mchezo wa kwanza kwake kufunga hat trick msimu wa 2024/25 akifikisha mabao matano ndani ya ligi.
ليست هناك تعليقات