Tazama Shape ya Mrembo Aliyekataa Milioni 50 ili Kufanya Tendo la Ndoa na Mwanaume
Wanaume wengi sana wanaamini kuwa hakuna mwanamke ambaye atakukataa endapo tu utampa pesa nyingi, kwani wanawake wamejawa na tamaa. Imani hii inawatafuna sana warembo ambao ni maarufu kwani wanaume mbalimbali hujitokeza na kuwahonga ili wafanye tendo la ndoa, lakini kwa Kidawa imekuwa tofauti kidogo.
Msanii wa Stive Mweusi anayefahamika kama Kidawa Matito aliwaeleza watangazaji wa Wasafi Fm katika kipindi cha Lavidavi kuwa, alikataa pesa kiasi cha shilingi milioni 50 kulala na mwanaume. Kidawa alieleza mengi sana juu ya swala hili lakin pia alifunguka kwanini alikataa pesa hizo nyingi ambazo anazitafuta kila kukicha.
"Nilikataa milioni 50 kutoka kwa mwanaume ambaye alitaka nilale naye" alisema Kidawa Matito kuwaambia watangazaji wa kipindi cha lavidavi pale Wasafi Fm. Kidawa aliongeza na kusema kuwa hakukataa kisa anamiliki pesa nyinga hapana, bali alikataa kutokana na utu ambao mwanaume huyo anao.
Kwa upande wa Kidawa Matito anaamini kuwa pesa sio kitu ambacho yeye anaweza kushawishika nacho kwani wanaume hao huwa wanapagawa na shepu yake. Alidai utu, kujali na upendo ndivyo vitamfanya afungue moyo na kumkabidhi mwanaume mwili wake. Kwaiyo huenda mwanaume mwingine asiwe na pesa lakini staili ambayo ataingianayo wakati anamfuata ndiyo itakayomfanya awe naye katika mahusiano.
Pia wewe kama ni msichana eiza uwe maarufu au sio maarufu, ni vizuri ukafuata maamuzi kama aliyoyachukua Kidawa Matito kwa kukataa pesa na kulinda utu wake. Kubadilisha mwili wako kwa pesa ni dhahili kuwa unajiuza na tabia ikikomaa basi utakuwa unaishi na kila mwanaume ambaye anakuonesha pesa ilimradi ku maokoto kwako yawe yanaingia.
Je una maoni gani juu ya wanaume ambao wanaamini pesa ndio kila kitu kwenye kumshawishi mwanamke?. Tuandikie maoni yako hapo chini pia usisahau kugusa neno Follow ili uwe wakwanza kupata makala zetu asante.
Chanzo: Wasafi Fm
ليست هناك تعليقات