WAKATI watani zao wa jadi Yanga wakiwa hawana muda wakupoteza ndani ya 18, mastaa wa Simba huwa wanapata kigugumizi wakiwa ndani ya 18 kwenye kumalizia nafasi ambazo wanazipata kujaza ndani ya nyavu.
Rekodi zinaonyesha kuwa timu namba moja kwa kufunga mabao mengi ndani ya 18 ni Yanga ikiwa inaongoza pia Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora.
Yanga baada ya mechi 20 ni maba0 42 wamefunga ndani ya 18 huku mabao 8 wakiwa wamefunga nje ya 18 kwenye msimu wa 2024/25 ikiwa na hatari zaidi pale inapokuwa na mpira ndani ya 18.
Kwenye dakika 1,800 ambazo Yanga imecheza imekuwa na wastani wa kuwa na hatari ndani ya 18 kila baada ya dakika 42 na kinara wa utupiaji ndani ya kikosi cha Yanga ni Clement Mzize mwenye mabao 10 na pasi nne za mabao. Jumla imefunga mabao 50.
Wakiwa ni namba moja kwenye utupiaji na vinara kwenye ligi wanafuatiwa na Simba ambao ndani ya 18 wametupia mabao 34 huku mabao manne wakiwa wametupia nje ya 18.
Simba kinara wa kucheka na nyavu ni mshambuliaji Leonel Ateba mwenye mabao 8 sawa na kiungo Jean Ahoua, ambapo wakali hawa kwenye mechi zilizopita walipokuwa ndani ya 18 walionekana kupata kigugumizi kwenye kumalizia nafasi.
Mchezo dhidi ya Fountain Gate, Ateba katika dakika za lala salama aligongana na mshikaji wake Steven Mukwala wakiwa ndani ya 18 kwenye harakati za kufunga na kwenye mchezo dhidi ya Prisons Ateba akiwa ndani ya 18 dakika ya 43 alikwama kutumia krosi ya Zimbwe Jr kupachika bao.
Licha yakuwa na kigugumizi kwenye kufunga bado Simba ni namba mbili kwenye timu zenye mabao mengi ndani ya ligi namba nne kwa ubora Afrika.
Azam FC mabao 24 imetupia ndani ya 18 huku mabao matano ikiwa imetupia nje ya 18 baada ya kufunga jumla ya mabao 29.
Timu zote zilizo ndani ya tatu bora, Yanga imeonekana kuwa na rekodi kali kwenye eneo la ufungaji iwe nje ya 18 ama ndani ya 18 balaa lake ni nzito ndani ya uwanja.
ليست هناك تعليقات