Subscribe Us

Breaking News

Lissu anaendekeza Umbea-Mbowe

 “Taarifa kwamba sikusema nilichozungumza na Rais ni umbea, na unapoona kiongozi mwandamizi kama kweli amesema..mimi sijasikikia ila kama kweli amesema inanishangaza kwasababu nimezungumza na Rais, tumezungumza na vyombo vya habari, nimeleta taarifa kamati kuu, kamati kuu imepeleka taarifa baraza kuu, baraza kuu lina wajumbe 500 kutoka mikoa na wilaya zote, wamekubaliana tuingie kwenye maridhiano, akisema hajui kilichozungumzwa wala hakuwa na taarifa ni umbea. Hiyo ni moja, mbili mimi nikiwa gerezani Rais alikwenda Brussels (Nchini Ubelgji) Makao Makuu ya Umoja wa Ulaya na akiwa huko alikutana na Makamu wangu, Mhe. Lissu wakazungumza na Lissu akamtaka Rais azungumze na CHADEMA, amuondoe Mwenyekiti gerezani na kadhalika, sasa yeye kuzungumza na Rais ilikuwa haki lakini Mwenyekiti wake kuzungumza na Rais imekuwa ni nongwa, hii siyo vizuri”

“Mimi ni Mwenyekiti wa chama yaani nikitaka kuzungumza na Rais wa taifa ni lazima niite mkutano mkuu, wajumbe wote kutoka kila jimbo nizungumze kuomba kibali cha Rais? Hapana, na katiba ya chama imenipa mimi mamlaka ya kuwa kiunganishi kati ya chama na serikali, ni majukumu ya Mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya chama, na mimi ndiye msemaji mkuu wa chama, hatuwezi kuwa na wasemaji wa chama kumi, lazima kiongozi mkuu ashike bendera na ndiye anakuwa msemaji mkuu wa chama”- Mbowe.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa na mgombea wa nafasi hiyo kwa mara nyingine Freeman Mbowe akizungumza siku ya Ijumaa Januari 17, 2025 katika kipindi cha Morning Trumpet kinachorushwa na chaneli ya runinga ya UTV.

No comments