Kesi ya uhaini dhidi ya Tundu Lissu kusikilizwa Mei 6,

Kesi ya uhaini inayomkabili mwenyekiti wa chadema Tundu lisu inatarajiwa kusikilizwa Mei 6 ambapo Lisu anawakilishwa na mawakili 31.
Siku hiyo inatarajiwa kuamuliwa ikiwa kesi hiyo itasikilizwa mahakani au kupitia mtandao.
Haya yanajiri baada ya polisi wenye silaha kuzingira nyumbani kwa Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanzania, chadema Tundu lisu pamoja na nyumbani kwa makamu mwenyekiti John Heche.
Hata hivyo Polisi hawajathibitisha kuzingira nyumba za viongozi hao wa Upinzani
Kupitia mtandao wa kijamii Heche ameandika “nimezingirwa nyumbani kwangu tangu saa kumi alfajiri ya leo, askari wakiwa na magari manne wako kwenye milango ya kuingilia” .
Haya yanajiri wakati mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hii leo inasikiliza upande wa Jamhuri(Mleta mashtaka) juu ya hoja za mawakili wa Lisu waliopinga kesi hiyo kusikilizwa kwa njia ya mtandao .
Polisi walisisitizia wanachama wa Chadema kutokwenda mahakamani wakisema ni kwa lengo la kuimarisha amani huku Makamu Mwenyekiti wa Chadema John heche akiwahamasisha wanachama wao kwenda kwani ni haki yao ya kikatiba.
Nje ya Mahakama ulinzi umeimarishwa huku Wanachama wa Chadema na waandishi wa habari wakiwa wamezuiwa kuingia mahakamani.
Tundu Lisu anakabiliwa na mashtaka mawili ya uchochezi kwa kutumia mitandao ya kijamii na uhaini ambapo kesi hiyo imepangwa kusikilizwa may 6.
Alikamatwa tangu April, 10, 2025 na yuko ndani kwa kesi ya uhaini ambayo haina dhamana.
Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa
app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii


No comments