BEKI wa kazi Wilson Nangu miongoni mwa wachezaji ambao wanavuja jasho ndani ya JKT Tanzania ambayo ipo ndani ya 10 bora anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Kariakoo ambao ni Simba.
Chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids kikosi cha Simba kimeruhusu mabao sita yakufungwa na katika hayo mawili wachezaji wa timu hiyo walijifunga, Ladack Chasambi dhidi ya Fountain Gate na Kelvin Kijili dhidi ya Yanga.
Katika eneo ambalo JKT Tanzania haijawa imara sana ni eneo la ushambuliaji ikiwa na wastani mdogo katika kucheka na nyavu baada ya mechi 19 safu ya ushambuliaji imefunga mabao 11.
Eneo ambalo imekuwa imara ni eneo la ulinzi ikiwa ndani ya timu tano bora ambazo zimefungwa mabao machache, JKT Tanzania ni namba tano ikiwa imefungwa mabao 15 ndani ya mechi 19.
Ndani ya dakika 1,710 ni mabao 15 imefungwa ikiwa na wastani wakufungwa bao moja kila baada ya dakika 114 huku ikiwa na wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika 155.
Ni timu ya kwanza kuambulia sare mbele ya Yanga baada ya ubao wa Meja Isamuhyo Februari 10 2025 kusoma JKT Tanzania 0-0 Yanga na mchezaji bora alikuwa ni Nangu.
Rekodi zinaonyesha kuwa Nangu aliokoa hatari zaidi ya 5 miongoni mwa hizo ilikuwa dakika ya 44, 45, 55, 68, 69, 73, 83, 90. Alicheza faulo ya hatari dakika ya 69 ikawa chanzo kwake kuonyeshwa kadi ya njano na mwamuzi Ahmed Arajiga.
Nangu alianza kikosi cha kwanza Februari 13 2025 wakati wakipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Singida Black Stars.
No comments