Bingwa wa Boda Boda Samia Cup kushinda ng’ombe na milioni 1

Mwenyekiti wa Vijana UVCCM tawi la Mikocheni A Hassan Yassin ameweka wazi kuwa mshindi wa mashindano ya Bodaboda Samia Cup atajishindia zawadi ya NG’OMBE na Shilingi milioni 1.
Mwenyekiti huyo ameyasema hayo katika uzinduzi wa michuano hiyo iliyofanyika jana February 7 katika Uwanja wa Michungwani Mikocheni A.
Aidha katika ufunguzi huo ilizikutanisha timu za Kidosho FC na Matozi wa kariakoo ambapo Matozi wa Kariakoo waliibuka na ushindi wa mabao 4-3.


No comments