Kitendawili kinachotia wasiwasi kuhusu ongezeko la saratani miongoni mwa vijana

Kuna visa vinavyoongezeka vya saratani ya matiti, utumbo mpana na saratani nyinginezo kwa watu wenye umri wa miaka 20, 30 na 40. Ni nini kinaendelea?
Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, viwango vya saratani ya utumbo mpana kati ya umri wa miaka 25 hadi 49 vimeongezeka katika nchi 24 tofauti, zikiwemo Uingereza, Marekani, Ufaransa, Australia, Canada, Norway na Argentina.
Matokeo ya awali ya utafiti huo, yaliyowasilishwa na timu ya kimataifa katika kongamano la ushirikiano wa kimataifa katika Kudhibiti Saratani (UICC) huko Geneva mnamo Septemba 2024, yalikuwa ya kushtusha.
Watafiti hao kutoka Shirika la Saratani la Marekani (ACS) na Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani chini ya Shirika la Afya Duniani (WHO) walitafiti data kutoka nchi 50 ili kuelewa mwenendo huo. Katika nchi 14 kati ya hizi, mwelekeo unaoongezeka ulionekana tu kwa watu wazima wenye umri mdogo, huku viwango vya watu wazima vikisalia kuwa thabiti.
Matokeo ni ya hivi karibuni zaidi katika tafiti nyingi zinazoelezea ongezeko sawa la aina mbalimbali za saratani kwa vijana.
Kwao na kwetu mara nyingi suala hili limevuka ufahamu, kwa sababu ni nani anayeweza kufikiria kuwa mtu mwenye afya njema mwenye umri wa miaka 40 angeweza kupata gonjwa hili hatari? - Eileen O'Reilly
Saratani ya matiti ni aina moja ya saratani ambayo mwelekeo wake umeweza kuonekana.
Ripoti mpya kutoka kwa ACS iligundua kuwa wakati vifo vinavyotokana na saratani ya matiti kwa wanawake vimepungua kwa karibu 10% katika muongo uliopita, viwango hivyo vinaongezeka kwa 1% kwa mwaka kwa ujumla - na 1.4% kwa mwaka kwa wanawake walio chini ya umri wa miaka 50.
Kulingana na uchunguzi wa epidemiological, inaonekana kwamba hali hii ilianza miaka ya 1990.
Utafiti mmoja uligundua kuwa wagonjwa wa saratani ya mwanzo yameongezeka kimataifa kwa 79% kati ya 1990 na 2019, na idadi ya vifo vinavyohusiana na saratani kwa vijana ikiongezeka kwa 29%.
Ripoti nyingine katika The Lancet Public Health ilielezea jinsi viwango vya saratani nchini Marekani vilivyoongezeka kwa kasi kati ya vizazi katika saratani 17 tofauti, haswa katika kizazi cha Xers na Milenia.
Suala la saratani zinazoanza mapema limekuwa jambo la kutia wasiwasi kiasi kwamba mashirika makubwa kama vile UICC yana nia ya kuongeza elimu kuhusu mwenendo huo miongoni mwa madaktari wa kawaida ili kuhakikisha kuwa dalili za tahadhari zinachukuliwa miongoni mwa wagonjwa wenye umri mdogo zaidi.
"Daktari anayemsikiliza mtu aliye na umri wa zaidi ya miaka 60 ambaye anazungumza juu ya ugumu wa kupata kinyesi, kuhisi uchovu na uvimbe, atachukua dalili hizo kwa umakini zaidi kuliko kijana aliye na miaka 30 ambaye yuko vizuri hata hali yake haiendani na hali ya kawaida wa mgonjwa saratani," anasema Sonali Johnson, mkuu wa UICC. "Wanaweza kuishughulikia kama ugonjwa wa akili unaotokana na hasira au msongo utokanao na kazi kwa hivyo kuna matukio mengi ambapo dalili za watu kutozingatiwa badala ya kufanyiwa uchunguzi zaidi wa damu au colonoscopy."
Wataalamu wa saratani wanasema kwamba wagonjwa wanaowasilisha magonjwa kama saratani ya kongosho, ugonjwa ambao watu wengi hugunduliwa mwanzoni mwa miaka 70, wakati mwingine huwa na miongo kadhaa kuliko inavyotarajiwa.
"Si kawaida kwangu kuona mtu aliye chini ya umri wa miaka 40 akiwa na saratani ya kongosho," anasema Eileen O'Reilly, daktari wa magonjwa ya saratani ya utumbo katika Kituo cha saratani cha Memorial Sloan Kettering huko New York. "Takriban kila wiki, jambo ni jambo la kuogofya. Hawa ni watu walio katika maisha ya ujana, ambao bado wanaanzisha familia na wana kila sababu ya kuishi. Athari kwa jamii ni kubwa."
Ingawa wataalam wa saratani kwa kawaida wamefikiria saratani kwa vijana kama matokeo ya hatari zinazoweza kurithiwa, kama vile mabadiliko ya vinasaba vya BRCA1 na BRCA2 katika suala la saratani ya matiti, wagonjwa zaidi na zaidi hawana mwelekeo dhahiri wa vinasaba.
O'Reilly anasema kwamba katika wagonjwa wengi ambao ni watoto wadogo,hakuna maelezo dhahiri ya kinasaba, na inaposomwa kwenye maabara, uvimbe unaobebwa na wagonjwa wenye umri wa miaka 20, 30 au 40 huonekana kuwa mkali zaidi ikilinganishwa na mgonjwa wa kawaida wa saratani ya kongosho katika miaka yao ya 70.
Anasema kwamba hii mara nyingi hufanya ubashiri wao huwa mbaya sana, ingawa mgonjwa mwenyewe mara nyingi huwa na afya njema.
"Kwa kuwa ni wachanga kiumri, wanafaa na mara nyingi wanaweza kushughulikia kiwango cha matibabu vyema, lakini wengine wana aina hii ya saratani ya kongosho, ambayo husababisha kudhoofika kwa kasi mbele ya macho yako," anasema "Kwao na sisi mara nyingi ni zaidi ya kufahamu, kwa sababu ni nani anayeweza kufikiria kuwa mtu mwenye afya njema mwenye umri wa miaka 40 atapata aina hii ya ugonjwa hatari?"
Pamoja na kutambua mwelekeo huo, wataalam wa saratani wanafikiri ni vema kuzingatia uharaka wa kujaribu kupata sababu zinazochangia hali hiyo.
Waandishi wa utafiti wa jarida la Lancet walitoa maoni kwamba ikiwa mtindo huu utaendelea, inaweza hatimaye kuongeza mzigo wa magonjwa katika siku zijazo, kusimamisha na hata kurudisha nyuma miongo kadhaa ya maendeleo ya afya ya umma katika kupambana na saratani.
Kwa hiyo ni nini kinaendelea?

Hata hivyo maelezo ya wazi zaidi yanaonyesha namna unene uliopitiliza na ugonjwa wa kimetaboliki, hali ambazo zimehusishwa na hatari ya saratani kupitia ongezeko la vichocheo mwilini na kusababisha kuharibika kwa njia kuu za homoni.
Utafiti wa hivi karibuni uligundua kuwa uzito wa mwili kupita kiasi kati ya umri wa miaka 18 na 40 kunahusishwa na hatari kubwa ya saratani 18 tofauti, wakati ripoti ya Lancet iligundua kuwa saratani 10 kati ya 17 ambazo zinakumba vijana nchini Marekani ni magonjwa yanayohusiana na unene wa kupindukia kama vile saratani ya figo, ovari, ini, kongosho na kibofu cha mkojo.
"Ushahidi wa jumla unaonyesha mabadiliko ya mtindo wa maisha," anasema Shuji Ogino, profesa katika Chuo Kikuu cha Harvard ambaye amekuwa akichunguza kuongezeka kwa saratani zinazoanza mapema. "Kila mmoja wetu ana maelfu ya vinasaba tofauti, ambavyo baadhi yake hutoa hatari ndogo sana ya saratani, ambayo huongezeka ikiwa ni pamoja na mabadiliko fulani ya mazingira. Tunajua kwamba kula sukari nyingi na vyakula vya kusindika, kuwa na viwango vya juu vya sukari mara kwa mara hufanya usugu sio tu huongeza hatari kupata ugonjwa wa kisukari bali pia saratani.
Lakini unene pekee hautoshi kukamilisha hili. O'Reilly anasema kwamba wagonjwa wengi wa saratani ya kongosho wenye umri mdogo anawaona wako sawa na wana afya nzuri, bila maelezo ya wazi kwa nini walipaswa kupata maradhi hayo. "Kwa hakika huwa inanishangaza kwamba mambo ya kitamaduni tunayofikiria zaidi hayatumiki kwa watu hawa," anasema. "Wanaonekana mara nyingi wenye afya njema kimwili ."
Ogino anaamini kwamba hii inaweza kuashiria kuibuka kwa baadhi ya vichocheo vya saratani mbalimbali, ambazo hapo awali zimevutia umakini mdogo. Ingawa wataalam wa magonjwa ya mlipuko wamezingatia kwa muda mrefu uhusiano kati ya uvutaji sigara na saratani, kiwango cha uvutaji sigara kimepungua sana katika miongo ya hivi karibuni huku WHO ikigundua kuwa ulimwenguni kwa sasa mtu mzima mmoja kati ya watano wanaotumia bidhaa za tumbaku sasa, ikilinganishwa na mtu mmoja kati ya watatu mnamo 2000.
Badala yake, Ogino anahisi kwamba uhusiano uliopuuzwa sana ni mabadiliko makubwa katika mifumo ya usingizi duniani kote ambayo yametokea katika miaka 50-100.
Utafiti mmoja uligundua kuwa wastani wa muda wa kulala wa watoto na vijana ulipungua kwa dakika 60 kila usiku kati ya 1905 na 2008, ilhali ufanyaji kazi kwa zamu umeongezeka sana katika miongo ya hivi karibuni huko Australia, China, Japan, Ulaya na Amerika Kaskazini na Kusini.
Utafiti wa 2021 kwa kutumia data za jarida la Kiingereza Longitudinal Study of Ageing, hifadhidata ambayo ina habari kutoka kwa zaidi ya watu 10,000 walio na umri wa zaidi ya miaka 50, ulipata uhusiano kati ya kukosa usingizi wa kutosha na hatari kubwa ya kupata saratani.
Wanasayansi wengine wamedai kuwa matumizi ya vifaa vinavyotoa mwanga kwa karibu kama vile vya kudumu na bandia, ama kupitia taa za barabarani au simu za rununu na kompyuta, huwakilisha saratani mpya kwa kusababisha usumbufu katika wa kibaolojia mwilini, kitu ambacho kimehusishwa na saratani ya matiti, koloni, ovari na tezi dume.
Uchunguzi umependekeza kuwa mwangaza unatumika wakati wa usiku kupitia shughuli zinazofanywa kwa zamu unaweza kuchangia ukuaji wa saratani kupitia kupunguza viwango vya homoni ya melatonin.
"Tunakabiliwa sana na matumizi ya mwangaza bandia wakati wa usiku, hata tangu tukiwa watoto," anasema Ogino. "Na huko Japani, kwa mfano, sehemu kubwa ya watu hukaa hadi usiku wa manane kila usiku.
Kazi ya kubadilisha fedha imekuwa ya kawaida zaidi na vitu kama vile maduka ya bidhaa ambayo hufanya kazi saa 24.
Wakati huo huo, Ogino anasema kwamba hakuna uwezekano wa kuwa na sababu moja ya hatari inayohusika katika visa hivi vya saratani inayoonekana mapema, lakini badala yake uhusiano wa sababu zinazobadilika zinazochangia ugonjwa huo.
Pamoja na mabadiliko ya mtindo wa maisha, watafiti wengi wa saratani wanaamini kuwa nguvu kuu ya magonjwa haya ni matokeo ya mabadiliko kadhaa ya sumu ndani ya utumbo.

Mnamo Juni 2023, Frank Frizelle, daktari wa upasuaji wa utumbo mpana katika Hospitali ya Christchurch, New Zealand, alitoa wito kwa wataalam wa saratani ya utumbo mpana kote ulimwenguni, akitaka uchunguzi wa kina wa uhusiano unaowezekana kati ya kula kiasi kikubwa cha plastiki ndogo na kusababisha saratani ya utumbo mpana.
Chapisho lake lililopewa jina, "Je! plastiki ndogo inaweza kuwa kichocheo cha saratani ya utumbo mpana?", alidai kuwa kuibuka kwa saratani ya utumbo mpana kama ugonjwa unaozidi kuwa shida katika miaka ya 50 inalingana na muda ambao microplastics zimepatikana kwa kasi zaidi katika mazingira.
Mapendekezo yake ni kwamba uwepo wa chembe hizi ndogo za plastiki zinaweza kuvuruga safu ya ute katika utumbo mpana, ambayo hulinda utando wa utumbo dhidi ya vimelea na sumu mbalimbali kutoka kwenye chakula.
Watafiti wengine wamependekeza kuwa vipengee fulani ndani ya vyakula vilivyochakatwa zaidi vinaweza kuchukua jukumu katika kuchochea uharibifu wa DNA ndani ya utumbo mpana, kutoka kwa rangi za chakula ingawa, kama ilivyo kwa microplastics, ushahidi bado unabaki mdogo.
Kwa sababu utumbo mpana umeunganishwa na tumbo na njia ya utumbo mpana na vile vile mfumo wa kinga, mabadiliko makubwa ndani ya utumbo hayahusiani na saratani ya utumbo mpana tu, bali pia aina mbalimbali za uvimbe ikijumuisha saratani ya matiti na saratani ya damu.
Watafiti wanachunguza ikiwa matumizi ya dawa za kuua viini 'antibayotiki' yanaweza kuwa sababu.
Hasa, dozi za 'antibayotiki' zinazotumiwa na watoto chini ya umri wa miaka mitano ziliongezeka kutoka 9.8 kwa kila watu 1,000 mwaka wa 2000 hadi 14.3 mwaka wa 2018.
Kwa ujumla, matumizi ya kimataifa ya kila mtu ya 'antibayotiki' ilikua katika makundi yote ya umri kati ya 2000 na 2015, kitu ambacho O'Reilly anaamini ni sababu kuu ya wasiwasi huo.
Katika miaka 10 iliyopita, Ogino na washirika wake duniani kote wamechapisha tafiti nyingi kuhusu baadhi ya vimelea nyemelezi ambavyo vinaonekana kuwa na uwezo wa kuvamia utumbo na kuendesha mabadiliko ya seli ambayo huongeza hatari ya kuendelea kwa saratani.


No comments