Rwanda yalaani vikwazo vya Marekani dhidi ya maafisa wake

Serikali ya Rwanda imelaani vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Waziri wa Rwanda anayehusika na Muungano wa Kikanda Jenerali Mstaafu James Kabarebe, ikimtuhumu kuhusika katika vita kati ya kundi la M23 na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Jenerali Kabarebe amewekewa vikwazo pamoja msemaji wa kundi hilo Lawrence Kanyuka.
Rwanda imekuwa ikishutumiwa kwa kuunga mkono kundi la M23, lakini inakanusha madai hayo.
Msemaji wa Serikali ya Rwanda, Yolande Makolo, alisema vikwazo hivyo havina msingi wowote na kusisitiza kwamba jumuiya ya kimataifa inapaswa kuunga mkono juhudi za kisiasa za mataifa ya kikanda kutafuta suluhu badala ya hatua alizozitaja kuwa "za kukatisha tamaa."
Aliongeza kuwa vikwazo haviwezi kuwa suluhisho la tatizo la muda mrefu mwashariki mwa DRC,na kama vikwazo vingetatua matatizo hayo ,eneo lingekuwa na amani miaka mingi iliyopita.

Marekani hapo jana ilitangaza vikwazo dhidi ya Jenerali Kabarebe, ambaye sasa ni Katibu wa Nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje, akihusika na ushirikiano wa kikanda.
Vikwazo hivyo ni vya kiuchumi, na pia vimewekewa msemaji wa kundi la M23, Lawrence Kanyuka.
Vikwazo vya Marekani dhidi ya afisa mkuu wa Rwanda vimefuatia kura ya Bunge la Umoja wa Ulaya, ambalo lilitaka Rwanda iwekewe vikwazo.
Rwanda imepinga vikali hatua hiyo na kukata ushirikiano wa kimaendeleo na Ubelgiji, ambayo ilishutumiwa kwa kuchochea vikwazo hivyo
ليست هناك تعليقات