Subscribe Us

Breaking News

Azam FC yaipigia hesabu AS Maniema kimataifa


UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa kwa sasa unaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo wao wa kimataifa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika ambapo wataanzia ugenini.

Azam FC saa 10:00 jioni watakuwa Uwanja wa De Martyrs kwenye kete yao ya kwanza katika anga la kimataifa ugenini Novemba 23,2025.

Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa tayari wanaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na kundi ambalo wapo kwa sasa.

“Maandalizi yanaendelea kwa kuwa mara baada ya mchezo wetu dhidi ya Namungo FC bado timu iliendelea na mazoezi, kikubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu ujao ambao hautakuwa mwepesi.

“Hatua ambayo tupo sio rahisi kutokana na kila timu kuona kwamba ina nafasi ha kupata matokeo mazuri, bado tunaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya AS Maniema Union,”.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kambini kwa maandalizi ya mchezo huo ni kiungo mgumu Sadio Kanoute ambaye aliwahi kucheza Simba SC, Legend Himid Mao, Jephte Kitambala.


Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa

                               app hii aipatikani google playstore kwa sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii 

No comments