Mamlaka nchini Kenya zimesema kwamba Watanzania wawili ni miongoni mwa watu 13 ambao wanaotuhumiwa kwa makosa ya kufadhili ugaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na wanakabiliwa na mashtaka na vile vile vikwazo vya kiuchumi.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa kwa vyombo vya habari nchini Kenya, Mamlaka zimesema kwamba watuhumiwa 13, wakiwemo Wakenya 10 na Mganda 1 na watanzania hao wawili wanachgunguzwa kwa kuhusika na shughuli za kigaidi ikiwemo ufadhili wake, na majina yao yameshawasilishwa kwa taasisi kama vile Benki na nyinginezo za kiusalama kuchunguza kwa kina vyanzo vya fedha walizonazo na jinsi fedha hizo zinavyotumika.
Hatua hiyo itazilazimu Benki husika kusimamisha akaunti za wahusika hao na kutoa taarifa muhimu kuhusu akaunti hizo kwa vyombo vya usalama nchini Kenya. Mashirika ya kutoa mikopo au huduma nyinginezo za kifedha zimeamrishwa kutofanya biashara na watu hao wakati huu ambapo uchunguzi kuwahusu inapoendelea.
Kamati maalum ya baraza la mawaziri inayochunguza ugaidi na ufadhili wake nchini Kenya imesema kwamba watu hao wanatakiwa kufungiwa akaunti zao za benki. Serikali ya Kenya kupitia kituo cha kuripoti uhalifu wa kifedha {Financial reporting centre} imeorodhesha majina ya 13 hao.
Watu aho ni Salehe Burhani Minja na Jerumani Koja kutoka Tanzania. Kutoka Kenya ni Violet Kemunto Omwoyo, Juma Ambare, Zakariya Kamal, Sufi Abasheikah, Jamal Abdi Mohammed na Hadija Issack Ali. Wengine ni Abdiweli Dubat Dege, Ramadhani Hamisi Kufungwa, Robert Karani Nyokae, Suena Nakhumicha Machabe, na Mohammed Siyat Ali huku mganda pekee ni Abubakar Swaleh.
Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa
app hii aipatikani google playstore kwa sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii

0 Comments:
Post a Comment