DIVA Amtetea Zuchu: Acheni Wivu, Zuchu ni Malkia wa Afrika Mashariki
Mtangazaji wa kipindi cha Lavidavi kinachorushwa Wasafi FM, @divatheebawse, amefunguka kwa hisia akimtetea msanii wa Bongo Fleva, Zuchu, dhidi ya maneno ya wivu na chuki kutoka kwa baadhi ya watu mitandaoni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diva ameandika:
"Sema watu mna wivu sana na roho mbaya... @officialzuchu is Number 1 Female Artist in East Africa, wivu tu... Acheni wivu na chuki! Kwenye kipaji na juhudi hakuna bahati, ni kazi halisi. Msanii huyu ndiye namba moja sasa Tanzania, show stopper wa ukweli!"
Zuchu, anayesimamiwa na lebo ya WCB Wasafi, amekuwa akiweka historia kwa kufikisha mamilioni ya streams kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki na kuandikisha rekodi za kipekee katika tasnia ya burudani Afrika Mashariki.
Kwa sasa, hakuna shaka kuwa Zuchu ameweka alama kubwa kwenye muziki wa Bongo Fleva na Afrika kwa ujumla, akithibitisha kuwa mafanikio yanahitaji juhudi, nidhamu na bidii ya kweli.
Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa
app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii

.jpg)

No comments