Gallery

2/07/2026


 Jon Hallford, mmiliki mwenza wa nyumba ya kuhifadhi maiti 'Mochwari' na kuzika inayoitwa “Return to Nature” huko Penrose, Colorado, amehukumiwa kifungo cha miaka 40 jela baada ya kubainika kuwa karibu maiti 200 zilihifadhiwa vibaya.

Hallford alitahadharisha Mahakamani na kusikia familia zikielezea hofu walizopata kuona wapendwa wao wakidhalilika chini ya huduma yake. Baadhi ya familia walimtaja Hallford kama “mtu katili” anayestahili kuangamia gerezani.

Mke wake wa zamani na mmiliki mwenza, Carie Hallford, amekiri makosa hayo pia na anasubiri hukumu.

Mochwari hiyo ilikuwa ikiwapa familia majivu bandia badala ya mabaki halisi ya wapendwa wao. Mahakama ilibaini kuwa maiti 189 zilihifadhiwa vibaya kwa zaidi ya miaka minne. Familia za ndugu wa marehemu zilizokusanyika mahakamani ziliomba apewe kifungo cha juu zaidi cha miaka 50.

Hallford alikiri makosa yake na kusema:

“Nilikuwa na fursa nyingi kuacha yote, lakini sikufanya. Makosa yangu yataendelea kuathiri vizazi vijavyo.”

Mawakili wa serikali walisema familia hiyo ilikuwa ina tamaa, huku ikiwa na uwezo wa kutunza maiti vizuri. Mochwari hiyo ilikuwa ikihifadhi maiti na kufanya mazishi bila kemikali, ikitumia jeneza linaloharibika haraka.

Vilevile, uchunguzi ulianza baada ya malalamiko ya harufu mbaya kutoka kwenye nyumba hiyo. Maiti zilizobainika zikiwa jumla ya 115 zilikusanywa mwanzoni mwa Oktoba mwaka uliopita.

Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa

                               app hii aipatikani google playstore kwa sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii 

0 Comments:

Post a Comment