Subscribe Us

Breaking News

RECAP: Zuchu kukutana na Ayra Starr ni hatua kubwa kwa muziki wake – El mando

 Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia Zuchu kukutana na staa wa Nigeria Ayra Starr Zanzibar.

Anasema kuwa Zuchu ameonyesha namna alivyo na malengo makubwa ya kimuziki, inawezekana hiyo Clip na Ayra Starr ya zamani lakini imekaa kimkakati zaidi.

Hiyo ni hatua kubwa sana kwenye muziki wake, kama watafanikiwa kufanya Collabo maana yake ni kwamba Zuchu ataingia moja kwa moja kwenye level za msanii wa Kimataifa kutokana na ukubwa wa Ayra Starr kwa sasa.

Zuchu anatakiwa ku-focus na kazi na sio kubishana na akina Juma Lokole, anatakiwa awe kwenye Tour za pamoja na Ayra Starr, Tems na Tyla ndio level zake.


No comments