
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga wamewapoteza watani zao wa jadi Simba kwenye eneo la ushambuliaji kwa kuwa na safu kali ya ushambuliaji ndani ya uwanja kwenye mechi za ushindani msimu wa 2024/25.
Baada ya kucheza jumla ya mechi 20 ambazo ni dakika 1,800 safu ya ushambuliaji ya Yanga imetupia mabao 50 ikiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 36 ndani ya uwanja kwenye mechi za ushindani.
Yanga ni timu namba moja ambayo imepata ushindi mkubwa kwenye mechi zake ikipata ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya KMC na iliwatungua mabao 6-1 Ken Gold kwenye mechi za ligi zote zilichezwa Uwanja wa KMC, Complex.
Wakati ikiwa namba moja kwenye ligi na pointi zake 52, watani zao wa jadi Simba wapo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa nit imu namba mbili kwa timu zenye mabao mengi imetupia mabao 41 baada ya kucheza mechi 19.
Katika dakika 1,710 ilizocheza imekuwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 41 ndani ya uwanja hivyo na kinara wautupiaji ni Jean Ahoua mwenye mabao 10 na pasi tano za mabao.
Mchezo pekee ambao Simba ilipata ushindi mkubwa ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar walipopata ushindi wa mabao 5-2 llikuwa Uwanja wa Kaitaba ikiandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza kupata ushindi mkubwa ndani ya msimu wa 2024/25 baada yah apo haijavunja rekodi yake hiyo.
Vita ni vikali kwa wababe hawa wawili ndani ya ligi namba nne kwa ubora ambapo kila mchezaji anapambania kuona timu inapata matokeo ndani ya uwanja kwenye mechi za ushindani.
Ni tofauti ya mabao 9 ambayo inawatenganisha wababe hao kwenye mbio za kutwaa ubingwa huku bingwa mtetezi akiwa ni Yanga anayeongoza ligi.
No comments