Subscribe Us

Breaking News

Mambo tisa kuhusu Lesotho - nchi ndani ya nchi

Wanawake waliovyaa magwanda ya kiasili, mavazi ya Basotho ya rangi tofauti wakiimba na kucheza

CHANZO CHA PICHA,AFP

Maelezo ya picha,Raia kutoka Lesotho wanafahamika kama Basotho
  • Author,

Serikali ya Lesotho imeshangazwa na kauli ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kwamba "hakuna aliyewahi kusikia kuhusu" taifa la Lesotho, lililopo Kusini mwa Afrika.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema ''hakuna aliyewahi kusikia kuhusu'' nchi iliyoko Afrika ya Lesotho - kauli ambayo ''imeshangaza'' serikali ya nchi hiyo.

Ni nchi ndogo iliyoko kusini mwa bara la Afrika ambayo ina milima mingi na imezungukwa na Afrika kusini pande zote.

Haya ni mambo tisa unapaswa kujua kuhusu nchi hii:

Pia unaweza kusoma:

1. 'Ufalme ulio juu ya milima'

Ufalme wa Lesotho umeundwa zaidi na nyanda za juu, na ufikiaji wa vijiji vingi nchini humo itakulazimu kutumia farasi, kutembea au uabiri ndege.

Inajulikana kama '' Kingdom in the Sky'' nchi huru pekee duniani ambayo yote iko juu ya mita 1,000 juu ya usawa wa bahari (UB) (ft 3,281).

Eneo la chini zaidi liko mita 1,400 (futi 4,593), na zaidi ya asilimia 80 za nchi ziko juu ya mita 1,800 (futi 5,906) kulingana na Encyclopaedia Britannica.

Inafahamika kuwa na mojawapo ya viwanja vya ndege vinavyotisha zaidi duniani kutua - Uwanja wa Ndege wa Matekane una njia fupi ya kurukia na yenye utuo mrefu kwenye ncha zote mbili.

Tovuti ya Business Insider inaelezea kuruka kutoka uwanja wa ndege ni sawa na wakati ndege anasukumwa kutoka kwenye kiota ili kujifunza kuruka".

2. Imezungukwa na Afrika Kusini pande zote

Lesotho inazungukwa kabisa na Afrika Kusini, ingawa imejitenga kutokana na milima kubwa.

Ardhi ya Lesotho haitumiki kwa kiwango kikubwa kwa kilimo, na wakazi wake hupata changamoto ya uhaba wa chakula, huku wakitegemea zaidi mapato yatokanayo na kazi katika taifa jirani la Afrika Kusini.

Kwa miongo mingi, maelfu ya wakaazi hulazimika kuhamia Afrika Kusini kutafuta ajira kutokana na ukosefu wa fursa za kazi nchini mwao.

Watu wa Lesotho, ambao ni zaidi ya milioni mbili, wana baadhi ya kanuni za utamaduni na lugha zinazofanana na za Afrika Kusini.

Lugha yao, Sesotho, ni mojawapo ya lugha rasmi 11 za Afrika Kusini.

Kwa kweli, kuna idadi kubwa zaidi ya wazungumzaji wa Sesotho Afrika Kusini – milioni 4.6 – kuliko taifa la Lesotho.

3. 'Rasilimali kubwa ya Lesotho ni 'dhahabu nyeupe'

Resources are scarce in Lesotho - a consequence of the harsh environment of the highland plateau and limited agricultural space in the lowlands.

Its biggest resource is water - known locally as white gold - which is exported to South Africa. Diamonds are another major export.

Rasilimali katika Lesotho ni chache, kutokana na mazingira magumu ya milima na ukosefu wa nafasi ya kutosha kwa kilimo kwenye maeneo ya chini.

Rasilimali kuu ya Lesotho ni maji, maarufu kama "dhahabu nyeupe," ambayo huuzwa Afrika Kusini.

Almasi pia ni bidhaa muhimu ambayo huuzia mataifa ya nje.

4. Ina kivutio kikubwa cha kuteleza kwa theluji katika jangwa la Sahara

Mtelezaji theluji akifanya mazoezi katika mteremlo wa Mlima Maluti ulioko Lesotho

CHANZO CHA PICHA,AFP

Maelezo ya picha,Wachezaji wa kuteleza kwa theluji kote ulimwenguni husafiri Lesotho katika eneo la AfriSki

Kama unapenda mchezo wa kuteleza kwa theluji au mruko wa skii, eneo la kwanza la kufanyia mchezo huo huwa ni Kaskazini Marekani au kwa mteremko wa theluji wa Ulaya.

Lakini Lesotho imejinadi zaidi katika michezo ya kuteleza kwa theluji.

Ina eneo kubwa zaidi la kufania mchezo wa kuruka theluji katika jangwa la Sahara la Afrika, miongoni mwa maeneo machache kama hayo bara zima la Afrika.

Eneo la Afriski iliyokaa mita 3,222 juu ya usawa wa bahari, imekuwa kivutio cha wageni kutoka Afrika na maeneo mengine duniani.

5. Raia wa Lesotho wanafahamika kama Basotho

Watu wa Lesotho wanajulikana kama Basotho.

Baadhi ya bidhaa zao za kitamaduni ni mablangeti yao mazito na kofia lililo na umbo la pia inayojulikana kama mokorotlo.

Kofia hii ni nembo ya kitaifa na inaonekana katikati ya bendera ya Lesotho.

Mablangeti ya Basotho hutengenezwa kwa sufi nzito na yamejaa michoro ya kipekee, kila moja ikielezea historia ya jamii yao.

Watu wa Lesotho wanavaa mablangeti haya kwenye matukio maalum na hupatia wageni kama zawadi.

Mwanamume aliyesimama akiwa amejifunika blangeti ya Lesotho akisubiri oicha akiwa miongoni mwa wakaazi waliokutana katika bwawa la Katse

CHANZO CHA PICHA,AFP

Maelezo ya picha,Watu wa Basotho wanajulikana kuenzi blangeti zao za kitamaduni

6. Ina idadi kubwa ya maambukizi ya HIV

Lesotho pia inakutana na changamoto kubwa katika kupambana na HIV, ikiwa na kiwango cha juu zaidi cha maambukizi duniani.

Takribani mmoja kati ya watu watano wazima wanaishi na VVU, na maambukizi ni ya juu zaidi kuliko nchi nyingi, ikiwa ni pamoja na majirani zake Namibia, Botswana na Eswatini.

Serikali ya Marekani imetenga kiasi cha karibu dola bilioni 1 tangu 2006 kusaidia kukabiliana na janga hili, ikiwemo kwa huduma za kinga, matunzo na matibabu.


7. Mwanamfalme Harry ana mpango wa msaada nchini Lesotho

Kama vile Uingereza, Lesotho ina ufalme wa kikatiba.

Ikiwa na maana kwamba japokuwa kuna familia ya kifalme, ina waziri mkuu aliyechaguliwa kuongoza serikali.

Mwanamfalme Seeiso- ndugu mdogo wa Mfalme Letsie III, ni rafiki wa karibu na mwanamfalme Harry wa Uingereza.

Wawili hawa walianzisha shirika la Sentebale, linalofanya kazi na vijana walioathirika na HIV/Aids katika jamii za Lesotho.

8. Huuza vitambaa vya aina ya jinzi kwa Marekani

Aina ya kitambaa kigumu cha pamba huhusishwa zaidi na Marekani Magharibi lakini siku za hivi karibuni, mavazi ya jinzi yanayovaliwa Marekani hutoka Lesotho.

Viwanda vyake vya kutengeneza mavazi, vimeunda jinzi kwa ajili ya chapa maarufu za Marekani kama vile Levi's na Wrangler.

Mwaka jana, Lesotho iliuza vitambaa na nguo zenye thamani ya dola milioni 237 Marekani kupitia Sheria ya ukuaji na Fursa ya Afrika( Agoa) ambayo mauzo yake hayatozwi ushuru nchini Amerika.

Imeorodheshwa kama bidhaa za thamani zilizouzwa Marekani kupitia mpango huo.

Hata hivyo viwanda vingi vya vitambaa na nguo vinamilikiwa na wachina na Taiwan.

Moshoeshoe II huvaa miwani, blangeti ya kitamaduni na Mokorotlo . Amepanda farasi na kushikilia kamba zake

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Aina ya kofia ya kitamaduni inayojulikana kama mokorotlo, ikiwa imevaliwa na aliyekuwa mfalme wa Lesotho Moshoeshoe II

9. Nchi iliyo na kiwango cha juu cha watu wanaojitoa uhai duniani

Asilimia 87.5 ya watu laki moja nchini Lesotho ujitoa uhai kila mwaka, hii ni kwamujibu wa Umoja wa Mataifa wa Shirika la Afya Duniani.

Takwimu hii ni kubwa mara kumi zaidi ya wastani wa dunia,na kinachowafanya watu kujitoa uhai ni vigumu kuelewa, sababu ni zaidi ya moja.

Wataalamu wanasema kuwa matumizi ya dawa za kulevya na pombe, ukosefu wa ajira, na upungufu wa huduma za afya ya akili ni baadhi ya sababu zinazochangia ongezeko hili la kujitoa uhai.

No comments