Subscribe Us

Breaking News

Zitto Kabwe atoa nzito usiyoyafahamu kuhusu Vita ya Rwanda na DR Congo

 Hakuna kabila linaitwa Watutsi wala Wahutu. Kabila lazima liwe na lugha yake. Hakuna lugha ya watusi. Watusi na Wahutu ni madaraja ya kijamii ( social classes). Madaraja haya utayakuta eneo lote la interlacustrine – Banyarwanda, Barundi, Baha, Banyankole, Bamushi, Basubi, Banyambo nk.

Je Jamii hizi zipo katika eneo linaloitwa sasa Kongo? Ndio. Himaya za Kirundi na Kinyarwanda zimekuwa Kongo miaka 500 kabla ya King Leopold kutwaa kilichokuja itwa Congo Free State na kabla ya mipaka ya Wakoloni ya mwaka 1884/1885.

Kabla ya Wakoloni kuja huku kwetu Himaya zetu zilikuwa zinavuka mipaka ya sasa. Ikiwemo Himaya ya Rwanda ( Rwanda Kingdom chini ya Mwami Rwabugiri ) ambayo ilikuwa maeneo yote ya Kivu ya Kaskazini na sehemu ya Kivu ya Kusini

Sultan wa Zanzibar kwa mfano alikuwa anatawala Mashariki ya Kongo kupitia bwana Tipu Tippu makao makuu yake yakiwa Kindu Jimbo la Manyema. Ndio maana eneo kubwa la mashariki ya kongo wanaongea Kiswahili, swahiliphone, kwa sababu lilitawaliwa na Maliwali waswahili.

Ulichoandika hapa ni kitu kinaitwa conspiracies na sio historical facts. Kwa maandiko yako utakuja kusema watu wa Katanga, Kalemie, Moba, Manono, Kindu, Bukavu, Uvira, Baraka nk sio wakongo kwa sababu ni Swahiliphones. Kama unawatambua swahiliphones kama wakongo, vile vile rwandophones ni wakongo pia.

Mzizi wa fitna ni raia wote kupata haki zao sawa na majirani waache kuleta mizozo Kongo.

Kwa hiyo ondoa neno ukweli mchungu na weka neno nadharia za kikonsipirasi!

No comments