Mashabiki wa Senegal waliokamatwa Morocco walikuwa wana “funga” siyo kufanya mgomo wa kuto kula, amesema wakili.
Mashabiki kumi na wanane wa Senegal ambao walikamatwa nchini Morocco kwa makosa ya kufanya “uhuni” wakati wa fainali za kombe la mataifa ya Afrika, walikuwa wamefunga na siyo kufanya mgomo wa kutotaka kula, mwansheria wao alisema siku ya Jumamosi.
Haya yanajiri baada ya waendesha mashtaka mjini Rabat kukanusha kuwa mashabiki hao walikuwa wakijizuia kula, wakisema kuwa wamekuwa “wakipokea chakula kama kawaida na mara kwa mara.”
Kundi hilo lilikamatwa tarehe 18 Januari, siku ya fainali yenye msisimko wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambako Senegal iliifunga Morocco bao 1–0 mjini Rabat.
Ijumaa, wakili wao Patrick Kabou alisema kuwa mashabiki hao walimwandikia barua wakisema watakuwa “wakifunga mfululizo hadi pale Mahakama za Morocco zitakapowapa fursa ya kuwasikiliza.”
Hata hivyo, Jumamosi, Kabou alisema kuwa wamekuwa wakila “chakula cha asubuhi pekee” kama njia ya kupinga kuzuiliwa kwao kabla ya kesi yao kusikilizwa.
Chanzo cha mahakama kilichozungumza kwa sharti la kutojulikana, kilisema kuwa mkuu wa gereza aliwaambia waendesha mashtaka kuwa watu saba kati yao hawakuhudhuria chakula cha mchana Ijumaa, lakini walikuwa “wamenunua chakula”, bila kufafanua jinsi walivyokipata.
Baadaye “walikula chakula cha jioni” katika kantini ya gereza, chanzo hicho kiliongeza.
Kavou alikuwa amesema kuwa mashabiki hao walimweleza kuwa bado “wanasubiri kufahamu mashtaka yanayowakabili.”
Dakika chache kabla ya kumalizika kwa mechi ya mwezi uliopita, baadhi ya mashabiki wa Senegal walijaribu kuingia uwanjani, huku wachezaji wa Senegal wakisimamisha mchezo kwa karibu dakika 20 kupinga penalti iliyotolewa kwa Morocco mwishoni mwa mchezo.
Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa
app hii aipatikani google playstore kwa sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii

0 Comments:
Post a Comment