Ifahamu Hospitali ya Roma inayomtibu Papa Francis

Nje ya hospitali ya Gemelli mjini Roma kuna sanamu kubwa ya mmoja wa wagonjwa wake maarufu, Papa Yohane Paulo II (John Paul II).
Imetengenezwa kwa marumaru nyeupe ya Carrara, inaonyesha papa katika miaka yake ya mwisho ya maisha yake h, akiwa ameshikilia msalaba , huku uso wake ukionekana kujaa maumivu.
Madaktari katika hospitali ya Gemelli walisaidia kuokoa maisha ya John Paul, baada ya kupigwa risasi katika jaribio la mauaji lililoshindwa katika uwanja wa Mt Peter mnamo Mei 1981.
Alifanyiwa upasuaji wa saa sita ili kuondoa risasi kutoka kwenye fumbatio lake.
Hii ni mara ya kwanza kwa Papa kutibiwa katika hospitali kubwa zaidi mjini Rome.
Miongoni mwa wagonjwa wa sasa wa hospitali hiyo ni Papa Francis, ambaye alilazwa wiki iliyopita akiwa na maambukizi ya mfumo wa kupumua. Amegunduliwa kuwa na homa ya mapafu katika mapafu yote mawili na mwishoni mwa wiki amegundulika pia ana tatizo la figo, lililo katika hatua za awali.

Katika kipindi cha miaka 25 ya upapa wake, John Paul alilazwa karibu mara 10, wakati mwingine akilazwa kwa muda mrefu. Alipata matibabu ya magonjwa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uvimbe wa tumbo, nyonga iliyovunjika na tracheotomy, wakati ugonjwa alipokuwa akiugua ugonjwa wa Parkinson uliokuwa umefikia kiwango cha juu.
Gemelli, ambayo ni hospitali ya mafundisho ya Kikatoliki, ilifunguliwa katika miaka ya 1960. Ikiwa na vitanda zaidi ya 1,500 vya wagonjwa, ni moja ya hospitali kubwa za kibinafsi barani Ulaya.
Hospitali hii iliyojengwa juu ya ardhi iliyotolewa na Papa Pius XI kwa mwanateolojia na daktari Agostino Gemelli mnamo mwaka 1934, imejulikana kama "Hospitali ya Papa."
John Paul II hata aliipa jina la utani "Vatican Three," na St Peter's Square kuwa Vatican One, na makazi ya papa huko Castel Gandolfo, Vatican Two.
Katika miaka ya 1980, Gemelli alianzisha kitengo maalum cha Papa, ambacho bado kinatumika leo.


No comments