Ruvuma kuenzi mashujaa wa Vita ya Majimaji

Wananchi mkoani Ruvuma wameombwa kujitokeza kwa wingi katika tamasha la kuwaenzi mashujaa wa Vita ya Majimaji litakalofanyika kuanzia Februari 23 hadi 27, mwaka huu.
Wito huo umetolewa na Kaimu Mhifadhi wa Makumbusho ya Majimaji Rose Kangu wakati akitangaza ratiba na matukio yatakayofanyika katika siku tano za tamasha hilo.
Kangu alisema kilele cha maadhimisho hayo itakuwa ndio siku rasmi ya kuwaenzi mashujaa walionyongwa na wakaloni wakati wakipigana vita hivyo.
Hata hivyo, alisema matukio kadhaa ya kielimu na burudani yatatangulia siku 4 za mwanzo.
Alisema siku ya Februari 23, kutakuwa na maonesho ya bidhaa za utamaduni ambapo watalii na wananchi kwa ujumla watapata fursa ya kujionea na kununua bidhaa hizo.
Kadhalika, siku hiyo wananchi watajifunza masuala ya utamaduni za watu wa mkoa wa Ruvuma ikiwemo nyimbo, lugha, lugha nk.
Siku inayofuata, Februari 24, makabila kutoka katika halimashauri zote 8 yatashindana katika ngoma za asili ili kupata washindi watatu watakaotumbuiza siku ya kilele.
Pia, kwa mujibu wa bi Kangu, siku hiyo kutakuwa na mashindano ya kupika vyakula vya asili na ujuzi wa dawa za asili.
Mhifadhi Kangu alisema Februari 25 kutakuwa na mdahalo mkubwa katika ukumbi wa shule ya Dkt Samia wilayani Namtumbo utahusu utamaduni wa makabila ya wilayani humo.
Kwa mujibu wa ratiba, Februari 26 itakuwa siku maalumu ya Wangoni (Ngoni Day) ambapo wananchi watakusanyika eneo la Maposeni ambako ilipo Ikulu ya Chifu wa Wangoni, Mputa Gama.
Mwenyeji wa mkusanyiko huo atakuwa Inkosi Emmanuel Gama, ambapo Watannzania watajifunza vipengele vya utamaduni wa wangoni ikiwemo chakula cha asili n.k.
Naye, Katibu wa Chama cha Mapinduzi Manispaa ya Songea James Mgego, amewataka viongozi wa chama huu hicho kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki katika tamasha hilo.
ليست هناك تعليقات