Tetesi za soka Ulaya Alhamisi: Real Madrid wako tayari kumnunua beki wa pembeni wa Liverpool Trent Alexander-Arnold

Real Madrid wako tayari kuongeza kasi ya kumsaka beki wa pembeni wa Liverpool Trent Alexander-Arnold, huku Los Blancos wakiwa na uhakika wa kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 26. (Telegraph – Subscription Required)
Mkufunzi wa Al-Hilal Jorge Jesus anataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah msimu huu wa joto, huku Mmisri huyo mwenye umri wa miaka 32 akikataa kandarasi mwishoni mwa msimu. (Daily Mirror)
Lakini matumaini ya kumsajili Salah kutoka Liverpool yanafifia miongoni mwa klabu za Saudi Arabia, ambazo zinahisi vinatumiwa kama mwafaka katika mazungumzo ya kandarasi. (I)
Liverpool inasisitiza kuwa mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, 25, hauzwi licha ya kutakiwa na Saudi Pro-League. (Mail – Subscription Required),


No comments