Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi: Atletico inafikiria kumsajili Jackson
Atletico Madrid waungana na Aston Villa na Newcastle kumsaka Nicolas Jackson, Paris St-German inamnyatia Ibrahima Konate, huku Newcastle pia ikiungana na Brentford na Brighton katika mbio za kuwania saini ya Nicolas Kuhn.
Atletico Madrid wanatafakari uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Nicolas Jackson msimu wa joto, huku Aston Villa na Newcastle pia zikimfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal, 23. (Sun)
Paris St-Germain wanavutiwa na beki wa Liverpool mwenye umri wa miaka 25 wa Ufaransa Ibrahima Konate, ambaye yuko tayari kuhamia Ligue 1. (ESPN)
Newcastle imeungana na Brentford na Brighton katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Celtic Mjerumani Nicolas Kuhn, 25. (Team Talk
No comments