Timu ya Taifa ya ngumi ya wanawake yakosa fedha za tiketi za Ndege kwenye Ulaya, yaomba msaada

Shirikisho la ngumi Tanzania (BFF) linahitaji jumla ya Sh. Milioni 166.9 kufanikisha kwa mafanikio ushiriki wa timu ya Taifa ya ngumi katika mashindano ya ubingwa wa Dunia kwa wanawake.
Mashindano hayo yanategemewa kufanyika nchini Serbia katika mji wa Nis kuanzia Machi 6 hadi 17 mwaka huu.
Pesa hizo zinazohitajika zitakamilisha gharama zote za kambi wakati wa mazoezi ya maandalizi pamoja na kukamilisha malipo ya safari ikiwa ni tiketi za ndege chakula na malazi wakiwa nchini Serbia, bima pamoja na posho.
Leo timu hiyo imeanza mazoezi rasmi katika chuo cha taaluma ya Polisi DPA kilichopo kurasini jijini Dar es salaam ikiwa na jumla ya mabondia 16 na makocha watatu baada ya kuongezwa katika kikosi hiko bondia Martha Patrick kutoka timu ya NGOME.
Kufanikiwa kushiriki kwa mashindano hayo italeta tija kwa maendeleo ya michezo Tanzania na kwa mabondia wanawake watakaoshiriki kwani kuna uwezekano wa kujikomboa kiuchumi hasa kutokana na zawadi watakazopata washindi wa mashindano hayo kwa jumla ya USD 2.88 milioni zilizoandaliwa kwa ujumla kwa mgawanyo kama ifuatavyo.
Medali ya dhahabu zawadi yake Dola za Marekani 100, 000 sawa na milioni 255 za kitanzania.
Medali ya fedha Dola za Marekani 50,000 sawa na milioni 126. 9 na laki tano za kitanzania
Medali ya shaba Dola za Marekani 25,000 sawa na milioni 63. 5 za kitanzania.
Tano bora Dola za Marekani 10,000 sawa na milioni 25. 4 za kitanzania.


No comments