Subscribe Us

Breaking News

Trump ametangaza mazungumzo yaliyopangwa na Ukraine na Urusi

 


.

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Rais wa Marekani Donald Trump amesema utawala mpya wa Marekani umepanga mazungumzo na Ukraine na Urusi, na majadiliano yanakwenda "vizuri sana," alisema.

"Tuna mikutano na mazungumzo yaliyopangwa na pande mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Ukraine na Urusi. Na nadhani majadiliano hayo yanakwenda vizuri sana," Trump aliwaambia waandishi wa habari, bila kufafanua zaidi.

Donald Trump hapo awali alizungumza juu ya utayari wake wa kufanya mazungumzo na Rais wa Urusi Vladimir Putin, lakini Kremlin inasema bado hakuna mapendekezo maalum yaliyopokelewa kutoka Washington.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, katika mahojiano na Associated Press mwishoni mwa juma, alitaja wazo la mazungumzo ya kumaliza vita bila ushiriki wa wawakilishi wa Ukraine kuwa hatari.

"Nadhani ni hatari sana, nafkiri, ikiwa kuna mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Marekani na Urusi kuhusu Ukraine bila Ukraine yenyewe. Hii ni hatari sana. Wanaweza kuwa na uhusiano wao wenyewe. Lakini kuzungumza kuhusu Ukraine bila sisi ni hatari kwa kila mtu,” alisema.

No comments