Subscribe Us

Breaking News

Uasi wa M23

 


j

CHANZO CHA PICHA,GÖKTAY KORALTAN / BBC

Maelezo ya picha,Mwandishi wa habari wa ndani anasema vyombo vya habari huko Goma vinajizuia katika hali ya kutokuwa na uhakika

M23 wanajitangaza kama wapigania uhuru, wanaoleta amani na utulivu katika nchi iliyovurugika, na kiongozi aliyeshindwa Rais wa Congo, Félix Tshisekedi.

Ni kundi la waasi, linalojumuisha watu wa kabila la Watutsi, na limekuwa likisonga mbele tangu mapema mwaka 2022, likiteka maeneo mengi - kwa msaada wa wanajeshi 4,000 wa Rwanda.

Hayo ni kwa mujibu wa wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaosema Rwanda ina "udhibiti wa mkubwa" juu ya kundi hilo - lakini Kigali na Rais wa Rwanda Paul Kagame wanakanusha.

Madhara ya kusonga mbele M23 yanaonekana katika Hospitali ya Ndosho, ambako Heshima inatibiwa.

Madaktari wanatatizika kuondoa mrundikano wa raia na wanajeshi waliojeruhiwa mwishoni mwa Januari, waasi walipouchukua mji wa Goma. M23 wanasema "waliukomboa" mji huo.

Idadi ya waliofariki katika mapigano hayo inakaribia watu 3,000, kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa.

Vyumba vinne vya upasuaji vinatumika kwa wakati mmoja - mchana na wakati mwingine usiku.

"Hali imekuwa mbaya kwa madaktari," anasema Myriam Favier wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC), ambayo inasaidia hospitali hiyo.

Madaktari hao wamekuwa wakilala katika vyumba vya upasuaji, anasema.

"Vifaa vyetu vya matibabu viliporwa mwanzoni kabisa mwa vita. Na tulikuwa na mmiminiko wa watu ambao haukutokea hapo awali - kati ya wagonjwa 100 na 150 kwa siku kwa wiki kadhaa."

Kwa sasa ni chini ya watu 10 kwa siku, kulingana na Bi Favier na sasa watu wanajaribu kurudi katika maisha yao

No comments