Subscribe Us

Breaking News

Uingereza yawakataa makomando 2000 wa Afghanistan

Vikosi vya Uingereza

CHANZO CHA PICHA,BEN TAGGART

Maafisa wa Vikosi Maalum vya Uingereza walikataa maombi ya kutaka kuhifadhiwa kutoka kwa zaidi ya makomando 2,000 wa Afghanistan waliowasilisha ushahidi wa kuaminika wa kuhudumu katika vikosi vilivyopigana bega kwa bega na SAS na SBS, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza (MoD) imethibitisha kwa mara ya kwanza.

Inaelezwa kuwa maafisa wa Vikosi Maalum vya Uingereza walikataa kila ombi kutoka kwa aliyekuwa komando wa Afghanistan yaliyowasilishwa kwao kwa ajili ya udhamini, licha ya kwamba vikosi hivyo vya Afghanistan vilipigana pamoja na Waingereza katika operesheni hatari dhidi ya Taliban.

Hapo awali, MoD ilikanusha kuwa kulikuwa na sera ya jumla ya kukataa wanachama wa vikosi hivyo – vinavyojulikana kama Triples – lakini BBC haijapata ushahidi wowote unaoonyesha kuwa Vikosi Maalum vya Uingereza (UKSF) viliunga mkono maombi yoyote ya makazi.

MoD ilipoulizwa ikiwa UKSF iliunga mkono au kukubali maombi yoyote, ilikataa kujibu swali hilo. Vikosi vya Triples vilivyopewa majina ya CF 333 na ATF 444, viliundwa, kupewa mafunzo, na kulipwa na Vikosi Maalum vya Uingereza, na vilisaidia SAS na SBS kwenye operesheni nchini Afghanistan.

Wakati nchi hiyo iliangukia mikononi mwa Taliban mnamo 2021, walitajwa kuwa katika hatari kubwa ya kulipiziwa kisasi na walistahili kuomba makazi na kuhifadhiwa nchini Uingereza.

Kukataliwa kwa maombi yao kulizua utata kwa sababu kulitokea wakati ambapo uchunguzi wa umma nchini Uingereza ulikuwa ukiendelea kuchunguza madai kwamba Vikosi Maalum vilitekeleza uhalifu wa kivita katika operesheni nchini Afghanistan ambapo vikosi vya Triples vilikuwepo.

No comments