Balozi wa Afrika Kusini 'hakaribishwi tena' ndani ya nchi yetu, Rubio anasema

Marekani inamfukuza balozi wa Afrika Kusini mjini Washington, huku Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio akisema "hakaribishwi tena katika nchi yetu bora".
Katika ujumbe kwenye mtandao wa X, Rubio alimshutumu Balozi Ebrahim Rasool.
Alimtaja kama "mwanasiasa mbaguzi", na kuongeza "hatuna cha kujadiliana naye".
Hatua hiyo isiyo ya kawaida inaashiria kilichoendelea hivi punde katika kuongezeka kwa mvutano kati ya nchi hizo mbili.
BBC imewasiliana na ubalozi wa Afrika Kusini mjini Washington DC kwa maoni yake.
Katika wake wa siku ya Ijumaa, Rubio alihusishwa na makala kutoka shirika lenye kuegemea mrengo wa kulia Breitbart ambalo lilinukuu baadhi ya matamshi ya hivi majuzi ya Rasool aliyoyatoa wakati wa mhadhara wa mtandaoni kuhusu utawala wa Trump.
"Anachoanzisha Donald Trump ni shambulio dhidi ya mamlaka iliyo madarakani, kwa kuendeleza ubaguzi dhidi ya mamlaka iliyo madarakani, nyumbani ... na nje ya nchi," Rasool alisema katika hafla hiyo.
Akijibu, Rubio alimwita Rasool "PERSONA NON GRATA," akirejelea msemo wa Kilatini wa "mtu asiyekaribishwa".
Ujumbe huo kutoka kwa Rubio ulitolewa alipokuwa akiondoka Canada kutoka kwa mkutano na mawaziri wa mambo ya nje.
Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa
app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii



No comments