Subscribe Us

Breaking News

M23, Serikali ya DRC kukutanishwa rasmi wiki ijayo Angola


cvy

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mazungumzo ya amani ya ana kwa ana baina ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na waasi wa M23 yanatarajiwa kuanza katika mji mkuu wa Angola, Luanda, tarehe 18 Machi, kwa mujibu wa raisi wa Angola katika taarifa iliyotolewa Jumatano.

Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika imekuwa ikijaribu kusimamia makubaliano ya amani ya kudumu na kupunguza mvutano kati ya Congo na jirani yake Rwanda, ambayo imekumbwa na tuhuma za kuunga mkono kundi la waasi.

Hata hivyo Rwanda inakanusha tuhuma hizo.

Angola ilitangaza Jumatano kuwa itajaribu kuweka mazingira ya mazungumzo ya moja kwa moja ana kwa ana.

Serikali ya Congo imekataa mara kwa mara kushiriki katika mazungumzo na M23, ambapo siku ya Jumatano ilisema kuwa imepokea mwaliko wa Angola lakini haikuthibitisha ushiriki wake.

Siku ya Jumatano, Tina Salama, msemaji wa Rais wa Congo Felix Tshisekedi, aliiambia Reuters kuwa serikali imepokea mwaliko kutoka Angola lakini haikuthibitisha ushiriki wake.

Kiongozi wa M23, Bertrand Bisimwa, aliandika katika mtandao wa X akijivunia kumlazimisha Tshisekedi kukaa kwenye meza ya mazungumzo, alisema kuwa ni "uamuzi pekee w kiungwana kutatua mgogoro wa sasa" ambao umeongezeka kwa kiasi kikubwa tangu Januari.

Waasi wamedhibiti miji miwili mikubwa ya mashariki mwa Congo tangu Januari, ikiwa ni ongezeko la mgogoro huo wa muda mrefu ulioanza kutokana na mchanganyiko wa mauaji ya kimbari ya 1994 ya Rwanda na harakati za kudhibiti rasilimali kubwa za madini ya Congo.

Serikali ya Congo imesema watu wasiopungua 7,000 wamefariki katika mapigano tangu Januari.

Zaidi ya watu 600,000 wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano tangu Novemba, kwa mujibu wa ofisi ya masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.

Nchi Jirani za DR Congo, ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini, Burundi, na Uganda, wana wanajeshi mashariki mwa nchi hiyo, jambo linaloleta wasiwasi kuhusu vita kamili vya kikanda vinavyofanana na vita vya Congo vya miaka ya 1990 na mapema 2000 ambavyo viliua mamilioni ya watu.


Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa

                               app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii 

No comments