Machifu, manduna wa Kingoni watakiwa kutumia vazi la asili kama fursa

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanal Ahmed Abbas amewataka Machifu na Manduna wa kabila la kingoni kutumia vazi la asili kama fursa ya kivutio cha utalii kwa jamii ya mkoa huo kwani jambo hilo litawapatia kipato na kukuza uchumi wa Taifa uhifadhi wa mambo ya asili na historia kwa ujumla.
Kanal Abbas ameyasema hayo wakati wa Maadhimisho ya siku ya wangoni yaliyofanyika Mkoani Ruvuma ambapo amesema kabila la wangoni ni miongoni mwa kabila lenye historia kubwa katika mapambano dhidi ya utawala wa ukoloni wa Wajerumani hususani kipindi cha mapigano ya vita ya majimaji.
Amesema kumbukizi hizo zinafanyika Kila mwaka, lakini ikiwa ni ishara ya kuwaenzi mashujaa 67 waliopoteza maisha yao kwaajili ya kuijenga Tanzania bora ya leo, ambapo watu sasa wanafaidi matunda ya mashujaa hao.
Katika hatua nyingine Kanal Abbas ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuboresha mazingira mazuri katika Makumbusho ya Majimaji na kuwa kivutio muhimu cha makumbusho na urithi wa kihistoria ndani Mkoa huo na Taifa kwa ujumla.
“Nimshukuru pia Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan, Chief Hangaya, kwa kazi kubwa na Nzuri anazofanya kwenye taifa letu kudumisha Mila sanaa na desturi kuwa sehemu ya kazi hivi. Lakini nipongeze wizara zenye dhamana kuhusiana na utalii, sanaa na utamaduni kwa kuyaratibu vyema mambo haya” amesema

Naye Mkurugenzi wa Makumbusho za Mali kale, Adelaide Sallema anasema kuwa wananchi wa Tanzania wanapaswa kuendelea kutunza na kuhifadhi urithi wa utamaduni na urithi wa asili kwa ajili ya vizazi vijavyo ili viweze kujua wametoka wapi.
“Kama inavyosema kauli mbiu
wananchi na watanzania kwa ujumla, tuendelee kuhifadhi maeneo yetu, tuendelee kuyatunza, tuendelee kuelimisha wengine kuhusu urithi huu wa utamaduni na urithi wa asili, ili vizazi vya sasa vipate kufahamu, tulikotoka wapi, tupo wapi na tunaenda wapi.”
“Kwahiyo ni muhimu sana kuendelea hii elimu kwa vizazi vyetu ambavyo tunaanini kabisa tusipowaelimisha siku hii ya leo, kesho tutakuwa na janga kubwa la kizazi ambacho hakijui hata kimetoka wapi”
Adelaide aliongeza kuwa Makumbusho ni sehemu ya kutunza na uhifadhi wa urithi wa utamaduni wakishirikiana na Mkoa, jeshi pamoja Mila na desturi
“Makumbusho sisi tunajishughulisha na uhifadhi wa urithi wa utamaduni wa asili”
Kila mwaka tunashirikiana na Mkoa, tunashirikiana na jeshi la wananchi wa Tanzania, tunashirikiana pia na baraza la Mila na desturi kwaajili ya kuhakikisha kuwa maadhimisho haya yanafanyika Kila mwaka. Kwa hiyo kama

Aidha Adelaide amesema, utunzaji wa asili na utamaduni ni chachu kubwa ambayo inaweza kusababisha amani.
“Sisi kama Makumbusho tuna kazi kubwa sana ya kuhifadhi huu urithi ambao tunaona tusipouhifadhi unaweza ukapotea na watoto watakapokuja hawawezi wakajua tulianzia wapi, hata sasa hivi, tunatunza tunaimarisha ili tuseme kwamba amani iendelee zaidi.”
“Kwahiyo ni muhimu sana kuendelea hii elimu kwa vizazi vyetu ambavyo tunaanini kabisa tusipowaelimisha siku hii ya leo, kesho tutakuwa na janga kubwa la kizazi ambacho hakijui hata kimetoka wapi”


No comments