Netanyahu asema mashambulizi dhidi ya Gaza ni 'mwanzo tu' huku mamia wakiripotiwa kuuawa

Israel "imeanza tena mapigano kwa nguvu zote" dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alisema Jumanne usiku.
Katika taarifa ya video, alionya kwamba "mazungumzo yataendelea tu chini ya mshambulizi" na kwamba "huu ni mwanzo tu".
Maoni yake yanajiri baada ya ndege za Israel kufanya mashambulizi makubwa ya anga dhidi ya kile ambacho jeshi lilisema ni malengo ya Hamas huko Gaza.
Zaidi ya watu 400 wameuawa katika mashambulizi hayo, wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas ilisema, na mamia ya wengine kujeruhiwa. Wimbi hilo la mashambulizi lilikuwa kubwa zaidi tangu kusitishwa kwa mapigano kuanza tarehe 19 Januari.
Usitishaji huo wa mapigano uliochukua muda mfupi ulikuwa umeendelea hadi sasa, lakini wimbi hili jipya la mashambulizi linaonyesha mipango ya kukomesha vita hivyo inaweza kuwa nje ya meza.
Mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo ya Beit Lahia, Rafah, Nuseirat na Al-Mawasi siku ya Jumanne yalivuruga amani ambayo watu wa Gaza walikuwa wakipitia tangu Januari, na hospitali kwa mara nyingine tena zimefurika na majeruhi.
Mashambulizi dhidi ya Gaza yamelaaniwa na Misri, mpatanishi katika mazungumzo hayo. Mashambulizi hayo ya anga ni "ukiukaji wa wazi" wa makubaliano ya kusitisha mapigano na yanawakilisha " hatari", alisema Tamim Khallaf, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo.
"Nilishtuka kwamba vita vilianza tena, lakini wakati huo huo, hii ndiyo tunayotarajia kutoka kwa Waisraeli," Hael mkazi kutoka Jabalia al-Balad aliambia idhaa ya BBC ya Kiarabu. "Kama raia, nimechoka. Tumeathiriwa vya kutosha - mwaka mmoja na nusu kwa hili! Inatosha," aliongeza.
Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa
app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii



No comments