SIMBA YACHOKA KUGOTEA ROBO FAINALI KIMATAIFA

AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wamechoka kugotea hatua ya robo fainali kwenye mashindano ya kimataifa hivyo watapambana kuvuka hatua hiyo.
Kwa sasa kikosi cha Simba kipo nchini Misri kwa maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wao wa kimataifa hatua ya robo fainali dhidi ya Al Masry mchezo unaotarajiwa kuchezwa Aprili 2 2025 na robo fainali ya pili inatarajiwa kuchezwa Aprili 9 2025 Uwanja wa Mkapa.
Ni Machi 28 msafara wa Simba ulikwea pipa kuibukia Misri huku kipa Aishi Manula akiwa hayupo kwenye msafara uliopo huko kutokana na kutokuwa fiti ni Ally Salim, Hussen Abel na Moussa Camara hawa watakuwa na jukumu kwenye eneo la mlinda mlango.
Ally amesema kuwa kwenye mashindano ya kimataifa wamekuwa na mwendelezo mkubwa kuishia hatua yar obo fainali jambo ambalo linawaumiza kwa kuwa hawavuki mbele hivyo watapambana kuvunja rekodi hiyo.
“Tumekuwa na mwendelezo wa kuishia katika hatua ya robo fainali mara nyingi, hii hatuifurahii kwa kuwa mwisho wa kujifunza sasa inatosha, mara ya kwanza ya pili yatatu mpaka tano bado ni robo fainali sasa tunahitaji kuvuka hatua hii hadi nusu fainali.”
Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa
app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii



No comments