Tetesi za Soka Ulaya: Barcelona na PSG zinamfukuzia Partey
Klabu za Barcelona, Paris St-Germain na Juventus zinavutiwa na kiungo wa Arsenal na Ghana Thomas Partey, 31, ambaye kandarasi yake itakamilika mwishoni mwa msimu huu. (Caught Offside)
Liverpool kumenyana na Barcelona katika kinyang'anyiro cha kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Ureno na klabu ya AC Milan Rafael Leao, 25. (Team Talk),
Bayern Munich wamepunguza bei ya Kingsley Coman, 28, ambaye anasakwa na Arsenal huku wakitarajia kumuuza mshambuliaji huyo wa Ufaransa msimu wa joto. (Bild - kwa Kijerumani)
Mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, 25, mwezi Januari aliiambia Liverpool kuwa anataka kukihama klabu hicho lakini ombi lake la kujiunga na klabu ya Al-Hilal ya Saudia lilipingwa. (Football Insider)
Tottenham wanaamini kuwa wako katika nafasi nzuri ya kumsajili kiungo wa Uingereza Tyler Dibling, 19, ambaye hajaridhishwa na mkataba mpya unaopendekezwa na Southampton. (Sportsport)
Manchester City wanataka kumsajili Jeremy Monga wa Leicester City lakini watalazimika kupitia mahakama ili kukubaliana ada ya fidia ya winga huyo wa miaka 15 wa Uingereza. (Sun)
Kikosi cha Pep Guardiola pia kinamfuatilia beki wa AC Milan na Ufaransa Theo Hernandez, 27. (Caught Offside)
Eric Dier, 31, anataka kusalia Bayern Munich hadi mkataba wake utakapokamilika msimu huu wa joto, lakini beki huyo wa zamani wa Tottenham na England anasubiri klabu hiyo kufanya uamuzi. (Florian Plettenberg),

Beki wa Manchester United na Uswidi Victor Lindelof, 30, anataka kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto na kurejea katika klabu ya zamani ya Benfica. (Record - kwa Kireno)
Mshambuliaji wa Uingereza Jack Grealish, 29, huenda akaondoka Manchester City msimu huu wa joto. (Mail)
Milos Kerkez, 21, anatarajiwa kuondoka Bournemouth msimu huu wa joto na Liverpool inamfuatilia beki huyo wa Hungary. (Fabrizio Romano)
Borussia Dortmund wanajiandaa kuondoka kwa winga Muingereza Jamie Gittens, 20, huku Chelsea, Liverpool, Manchester United na Tottenham zikimuwania. (Sky Germany - kwa Kijerumani)
West Ham wanaweza kuwapa changamoto Newcastle kuinasa saini ya mshambuliaji wa Strasbourg Mholanzi Emanuel Emegha, 22. (GiveMeSport),



No comments