Subscribe Us

Breaking News

TMA yatangaza uwepo wa kimbunga ‘JUDE’ Bahari ya Hindi, kusababisha ongezeko la mvua

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza kuwepo kwa kimbunga Jude katika Bahari ya Hindi eneo la Rasi ya Msumbiji na kwamba kutokana na mwelekeo wa umbali wake hakitarajiwi kuwa na athari za moja kwa moja hapa nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TMA leo Jumatatu ya Machi 10, 2025, imeeleza kuwa kupitia uchambuzi  wa mifumo ya hali ya hewa unaonesha kuwa kimbunga hicho kitaingia nchi kavu katika eneo la Msumbiji mchana wa leo Machi 10, 2025 na kupungua nguvu yake.

“Hata hivyo, Kimbunga “JUDE” kinatarajiwa kurejea tena baharini na kuimarisha nguvu yake katika kipindi cha kati ya tarehe 13 hadi 15 Machi 2025. Aidha, kutokana na mwelekeo na umbali wake Kimbunga hicho hakitarajiwi kuwa na athari za moja kwa moja hapa nchini,” imeeleza taarifa hiyo

Kwa mujibu wa TMA imesema uwepo wa kimbunga hicho katika eneo la Rasi ya Msumbiji unatarajiwa kuchagiza mifumo ya hali ya hewa hapa nchini na kusababisha ongezeko la mvua katika maeneo mbalimbali. Vilevile, uwepo wa kimbunga hicho unaendana sambamba na kuanza kwa msimu wa mvua za Masika, 2025 katika maeneo yapatayo misimu miwili ya mvua kwa mwaka kama ilivyotabiriwa awali na taarifa kutolewa kwa Umma.

Taarifa hiyo imewashauri  watumiaji wa bahari na jamii kwa ujumla kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam wa kisekta.

“TMA inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga “JUDE” na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini na itaendelea kutoa taarifa 



Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa

                               app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii 

No comments