Subscribe Us

Breaking News

Waumini wa dini wanaoamini katika kufunga hadi kufa

h

CHANZO CHA PICHA,PRANAY MODI

Maelezo ya picha,Sayar Devi wakati wa mfungo wake wa mwisho

Wiki tatu baada ya kugundulika kuwa na saratani ya shingo ya kizazi, Sayer Devi Modi mwenye umri wa miaka 88 aliamua kutotafuta matibabu. Badala yake, alichagua kufunga hadi kufa.

"Ripoti yake kuhusu kipimo cha ugonjwa cha biopsy ilikuja tarehe 25, 2024 na kulingana na ripoti hhiyo , saratani ilikuwa inaenea. Julai 13, 2024, alikumbuka dini yake na kunywa supu. Baadaye, alituita na kuelezea wazo lake la kufunga hadi kufa, kifungo kinachoitwa (Santara) ," anakumbuka mjukuu wake, Pranay Modi.

Pia kifungo hicho hujulikana kama 'Salekhna', hii ni ibada inayofanywa na baadhi ya wafuasi wa dini ya Jain, ambapo mtu anajinyima chakula na maji na kukumbatia kifo.

Si jambo la lazima katika dini hii, na ripoti za vyombo vya habari vya India zinakadiria kwamba idadi wafuasi wa dini ya Wajaini, kati ya watu 200 na 500 kila mwaka, huchagua njia hii ya kifo.

Ujaini ni nini?

g

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Wajaini wanamuamini Mahavira, mwalimu wa karne ya 6, ambaye ndiye mwanzilishi wa dini ya kisasa.

Kutokuwa mtu wa ugu ni msingi wa Ujaini, dini ambayo ilianzishwa takriban a miaka 2,500 iliyopita. Ingawa hawana mungu, Wajaini wanaamini katika nafsi safi, ya kudumu, ya mtu binafsi, na inayojua yote.

Wajaini wengi ni walaji wa mboga na huweka mkazo mkubwa juu ya maadili ya na kukataa starehe za ulimwengu.

Kuna Wajain wapatao milioni tano nchini India, na wengi wao wameelimika sana. (Kituo cha Utafiti cha Pew chenye makao yake nchini Marekani kinasema kwamba thuluthi moja ya watu wazima wa Jain wana shahada ya chuo kikuu, ikilinganishwa na 9% ya idadi ya jumla ya Wahindi.) Pia, wengi ni matajiri kiasi.

Waalimu wa dini ya Jain mara nyingi huheshimiwa katika jamii pana ya Kihindi.

Waziri Mkuu Narendra Modi pia alikuwa aaliweka ujumbe wake wa X akielezea huzuni yake juu ya kifo cha mwalimu mmoja maalum, yaani Acharya Shri Vidyasagar Ji Maharaj, akielezea kifo chake kama "hasara isiyoweza kurekebishwa kwa nchi".

Mwalimu huyu, ambaye alikuwa amefunga siku tatu, alikuwa na umri wa miaka 77 alipofariki. Maelfu ya watu walihudhuria mazishi yake.

Wajaini wanasema kuwa mchakato huu wa kuhitimisha maisha ya mtu kwa kufunga hadi kufa haupaswi kulinganishwa na kujiua kwa kusaidiwa, ambacho ni i kitendo cha kuua mgonjwa kwa ugonjwa usioweza kupona na maumivu.

"Kujiua kwa kusaidiwa ni tofauti na kujiua kwa daktari kwasababu unasaidiwa na daktari na hakuna kumeza au kudunga kitu chochote chenye hatari," Stephen M. Voss, profesa msaidizi katika Chuo Kikuu cha Colorado-Denver na mtaalamu wa Ujaini, aliiambia BBC.

Ushahidi wa kihistoria wa kitendo hiki , kama ulivyoelezwa na Profesa Voss, yaani "kutoa mwili" au "kuruhusu mwili kudhoofika," ulianzia karne ya 6.


Kusherehekea maisha

g

CHANZO CHA PICHA,PRANAY MODI

Maelezo ya picha,Sayer Devi akiwa amelala kwenye sofa wakati wa mfungo wake wa mwisho, akiwa amezungukwa na wanafamilia yake

Imani katika karma, nafsi, kuzaliwa upya, na wokovu ni vipengele muhimu vya kifo hiki cha Santhara.

Baadhi ya Wajaini, kama vile Sayar Devi, huchagua kifo hiki wanapotambua kwamba kifo chao kiko karibu au baada ya kugunduliwa kuwa na ugonjwa usiotibika.

Katika video zilizochukuliwa wakati wa mfungo, Sayar Devi anaonekana akiwa amevaa sari nyeupe na kuziba mdomo wake na kipande cha mraba cha kitambaa.

"Alikuwa mtulivu, akiongea kwa ufahamu hadi mwisho," anakumbuka Pranay Modi.

Modi anasema kwamba wakati wa mfungo wa mwisho wa bibi yake, sherehe zilichukua sura mpya kwani watu wengi walikusanyika kwenye kaburi la Kabridham, katikati mwa India.

"Haikuonekana kama mahali ambapo mtu angekufa. Wanafamilia, jamaa, marafiki, majirani, na wageni wote walikuja kupokea baraka zake."

Hata katika siku zake za mwisho, mungu huyo wa kike alikuwa na nguvu za kufanya hija ya Jain iliyochukua kama dakika 48.

"Hakuna shaka alikuwa na uchungu mwingi baada ya kuacha kutumia dawa. Lakini hakulalamika kuhusu hilo. Uso wake ulikuwa unameremeta na amani."

Watoto na wajukuu wa Devi walitazama jinsi maisha yake yalivyokuwa yakififia hadi kufa.

"Inasikitisha sana kwangu kumuona akifa hivi," Modi anasema. "Lakini najua anaenda mahali pazuri zaidi. Tuliheshimu uamuzi wake."

Maumivu ya mwisho

g

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Miili ya watu wanaokufa kufuatia kutokana na kifo cha Santhara huchomwa wakiwa wamekaa.

Si mara zote kifo cha Santara huwa na mwisho wa amani. Nadharia ya udaktari ya Profesa Mickey Chase ilikuwa juu ya mada hii, na alikuwa ameona idadi kubwa ya watu waliokufa kifo hiki karibuni.

"Mwanamume mmoja ambaye alikuwa mgonjwa mahututi na saratani alipitia maumivu makali alipoanza kufanya mfungo wa Santhara. Ingawa familia yake ilijivunia matendo yake na kumuunga mkono, ilipata ugumu kumwona akiteseka," anasema Chase, profesa msaidizi katika Idara ya Mafunzo ya Jain katika Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison na Mwenyekiti wa Sri Ananthanath.

Katika tukio jingine, Chase aliona mwanamke aliyegunduliwa na saratani ya mwisho akiwa mtulivu baada ya kufunga.

"Tulihisi kuwa ni jukumu letu kama familia kumtia moyo na kuweka azimio lake imara, na hivyo waliimba nyimbo kwa ajili yake ambazo zilikuwa na uponyaji wa kiroho."

Profesa Voss anaamini kwamba kukabili matatizo fulani ni jambo lisiloepukika.

"Kuangalia mtu akifa kwa njaa haipendezi kwa njia yoyote. Nyakati za mwisho pia zinaweza kuwa chungu. Mwili unapopigana ili kujiokoa, mtu anaweza hatimaye kuomba chakula au maji. Lakini hii ni kawaida kutambuliwa kama sehemu ya mwisho," anasema.

Kwa njia hii, picha za marehemu watawa wa Digambar (watu wanaozurura uchi) zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha mashavu yao yakiwa yamezama na mifupa ya makalio yao ikibaki bila mwili. Ni kiashiria wazi cha njaa na upungufu wa maji mwilini.

Inaaminika kuwa wengi wa wale wanaochagua kufa kwa kufunga ni wanawake. Profesa Voss anaamini kuwa hii inatokana na wanawake kuchukuliwa kuwa wacha mungu zaidi na uwezo wao wa kuishi kwa muda mrefu kuliko wanaume.

Jamii hii inaona kifo cha kufunga hadi kufa -Santhara kama "mafanikio makubwa ya kiroho," anasema Profesa Chase.

Msingi wa kitheolojia ( mafundisho ya kidini)

g

CHANZO CHA PICHA,KAMAL JAIN

Maelezo ya picha,"Kwa kufunga na kukikubali kifo, mtu anaweza kutakasa mwili na roho na kupunguza karma mbaya kwa maisha bora ya kiroho katika kuzaliwa tena," anaelezea Maharaj Ji, mtawa mwingine.

Sri Prakash Chand Maharaj Ji (aliyezaliwa 1929) ni mtawa mkuu wa Jain wa Svetambara Nikaya. Svetambara inamaanisha kuvaa nguo nyeupe. Aliingia katika maisha ya utawa mnamo 1945. Baba yake na kaka yake mdogo pia wakawa watawa na kufuata kifo cha Santhara.

"Sikuwa na huzuni nilipomwona baba na kaka yangu. Nilijitenga kabisa. Sikuhisi kama ninakuwa yatima au kwamba kungekuwa na nafasi tupu maishani mwangu."

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 95 anaishi katika nyumba ya watawa katika mji wa Gohana kaskazini mwa India. Hatumii simu wala kompyuta ndogo na alizungumza na BBC kupitia mwanafunzi wake, Ashish Jain.

"Dhana ya kifo kizuri kama mwisho kamili wa maisha haya na mwanzo mzuri wa siku zijazo inategemea kanuni zangu za kifalsafa, kiroho na kidini," aliiambia BBC.

Mtawa huyu anasema kwamba mazoezi ya Santhara yanahusisha nyakati nyingi na hayawezi kufanywa ghafla au kwa msukumo. Mtu anahitaji ruhusa ya familia na mwongozo kutoka kwa walimu wa kiroho kama Maharaj Ji kwa hilo.

Hatua ya kwanza ya Santhara ni kufikiria kwa kina kuhusu dhambi na makosa yako yote ya zamani na kuyakubali. Kisha unapaswa kuomba msamaha.

"Kwa kufunga na kukumbatia kifo, mtu anaweza kutakasa mwili na roho na kupunguza karma mbaya kwa maisha bora ya kiroho katika kuzaliwa tena," Maharaj Ji anaelezea.

"Hatimaye itaisha na ukombozi wa roho kutoka kwa mzunguko wa kuzaliwa na kifo."

Changamoto ya kisheria

Desturi hiyo ilipigwa marufuku na Mahakama Kuu ya jimbo la kaskazini-magharibi mwa India la Rajasthan mwaka wa 2015, lakini uamuzi huo ulibatilishwa na Mahakama ya Juu Zaidi.

Aliyekuwa mtumishi wa umma D.R. Mehta ni mshiriki wa kesi iliyowasilishwa kulinda mila ya Santhara.

"Wajauni wanaona hii kuwa njia bora ya kufa. Ni kukubali kifo kwa fahamu, kwa amani na heshima. Utakaso wa kiroho na amani ya milele ndio nia kuu," anasema Mehta, ambaye ameshikilia nyadhifa kama vile naibu gavana wa Benki Kuu ya India na mwenyekiti wa Bodi ya Dhamana na Ubadilishanaji wa Fedha ya India.

Upinzani dhidi ya mila hiyo uliibuka tena mnamo 2016 kufuatia kifo cha msichana wa miaka 13 huko Hyderabad. Alikufa baada ya kufunga kwa siku 68, lakini wengine wote ambao waliofuata kifo cha Santhara katika miaka ya hivi karibuni wamekuwa wazee.

h

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Baadhi ya maandishi ya zamani zaidi kuhusu Santhara yanaweza kupatikana katika eneo hili la hekalu lililoko Karnataka.

Maharaj Ji alianza mchakato wa Salekhna mnamo 2016, ambao unatangulia ibada ya Santhara. Hapo awali alikuwa na vyakula kumi tu, sasa anaishi kwa vyakula viwili tu, maji, na dawa. Hata hivyo, bado yuko hai.

"Yeye haumwi au kuwa dhaifu. Huwa mwenye furaha kila wakati. Haongei sana," asema mwanafunzi wake Ashish Jain.

Maharaj Ji anaamini kwamba maisha yake ya upole yalimsaidia kufanya maendeleo ya kiroho.

"Nafsi yangu ya ndani na akili huhisi furaha sana. Niko katika hali ya furaha."




Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa

                               app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii 

No comments