Subscribe Us

Breaking News

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YAFANIKIWA KUTATUA MIGOGORO 136 MKOANI ARUSHA.

Mkurugenzi   huduma za msaada wa kisheria kutoka wizara hiyo Ester Msambazi akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha .
  
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .Wizara ya katiba na sheria imefanikiwa kutatua migogoro 136 kati ya migogoro zaidi ya  Mia sita waliyoipokea katika kampeni ya msaada wa kisheria wa  Mama Samia legal  Aid  inayoendelea jijini Arusha katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Hayo yamesemwa mkoani Arusha na  Mkurugenzi   huduma za msaada wa kisheria kutoka wizara hiyo Ester Msambazi  wakati akitoa  tathmini  kuhusiana na mafanikio  waliyoyapata toka waanze kampeni hiyo machi 1 ikiwa ni kuelekea siku ya wanawake duniani.
Amesema kuwa hadi kufikia leo  wameweza kufikia wananchi 1844  huku wengi wao wakiwa ni wanaume ndio wamekuwa na mwitikio mkubwa katika migogoro hiyo.
Msambazi ametaja kuwa migogoro iliyoongoza ni migogoro ya ardhi ikifuatiwa na migogoro ya madai tofauti na mikoa mingine ambapo mingi baada ya ardhi inafuatiwa na  masuala ya ukatili wa kijinsia na mirathi lakini kwa  Arusha wameona migogoro mingi ya madai.

“Kwa hizi siku saba tulizokuwa hapa tumeweza kuwafikia wananchi 1844 na tumepokea migogoro 677 na kati yake tumefanikiwa kutatua migogoro 136 kwa kuwapatanisha na kutatua changangamoto zilizokuwa zikiwakabili,” amesema Msambazi

“Migogoro mingi imewasilishwa na wanaume, inawezekana wanaume wana changamoto zaidi kuliko wanawake lakini pia inawezekana wamebeba  changamoto hizo kama baba wa familia ndio maana tumeona wengi wamejitokeza kuziwasilisha,”amesema .

Amefafanua kuwa  asilimia kubwa wamefanikiwa kuitatua kwa pande zote mbili kuweza kukaa na kukubaliana na lile lengo ambalo kama serikali walipanga kulifikia limefanikiwa kwa sehemu kubwa na mingine inaendelea, kwani kuna zilizopo mahakamani lakinj  mingine wanashughulikia kiutawala na itaendelea kufuatiliwa na yote itahitimishwa kwa jinsi ilivyo wasilishwa.

Ameongeza kuwa, wamewapa elimu juu ya  msaada wa kisheria lakini pia kutatua migogoro ambapo wamemetumia nafasi hiyo  kuwaandikia makubaliano, kuwawasilisha mahakamani wale ambao migogoro yao ilikuwa ina uhutaji wa kwenda mahakamani kwasababu kampeni imewajumuisha wadau kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo mawakili wa kujitegemea.

Msambazi amesema kuwa, lengo la kampeni hiyo ni kuhakikisha wanawa elimisha wananchi katika ngazi za kijamii kuhusiana na masuala mbalimbali ya kisheria na namna gani wanaweza kuifikia haki na kutatua migogoro ambapo hadi kufikia february 25,2005 wameshatekeleza kampeni hiyo mikoa 22.

Nao.baadhi ya wananchi  waliojitokeza katika kampeni hiyo na kutatua migogoro yao wamemshukuru Rais Samia kwa kuleta wataalamu.wa kutatua migogoro ya ardhi  mkoani Arusha ambapo wameweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa na kuomba zoezi hilo like linaletwa mara kwa mara kwani wananchi wengi wanateseka na hawana pa kukimbilia .




Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa

                               app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii 

No comments