Subscribe Us

Breaking News

JKT TANZANIA WAISUBURIA YANGA NUSU FAINALI

WAJEDA JKT Tanzania wanasubiri mshindi wa mchezo wa hatua ya robo fainali ya Aprili 15 2025 kati ya Yanga dhidi ya Stand United unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex.

Ikumbukwe kwamba JKT Tanzania inaingia kwenye orodha ya timu pekee iliyoambulia sare mbele ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika baada ya dakika 90 ubao ulisoma JKT Tanzania 0-0 Yanga katika mchezo wa ligi na Nangu alichaguliwa kuwa mchezaji bora.

Kwenye hatua ya robo fainali JKT Tanzania walipeleka kichapo cha kizalendo kwa wapinzani wao Pamba Jiji kwenye mchezo uliochezwa Aprili 14 2025 baada ya dakika 90 ubao ukasoma JKT Tanzania 3-1 Pamba Jiji.

Ipo wazi kwamba Yanga ni mabingwa watetezi pia wa taji hili ambapo wataingia uwanjani saa 10:00 jioni kusaka ushindi ndani ya dakika 90 ambao hata Stand United nao wanahitaji, hivyo mshindi wa mchezo wa leo atakutana na JKT Tanzania kwenye hatua ya nusu fainali.

Ni mabao ya Mohamed Bakari aliyefunga mawili na Yunus Lema alijifunga na bao la kufutia machozi kwa Pamba likifungwa na Henry Msabila ndani ya dakika 90.

Watani wa jadi wa Yanga ambao ni Simba tayari wamekata tiketi ya nusu fainali na wanatarajiwa kumenyana na Singida Black Stars iliyopata ushindi kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar mabao 2-0 Uwanja wa Liti, Aprili 14 2025.



Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa

                               app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii 

No comments