Maneno Aliyosema Ali Kamwe Baada ya Simba Kuingia Fainali CAF
Alikamwe ameumia, hivi ndivyo unavyoweza kueleza mara baada ya afisa habari huyo wa klabu ya Yanga Sc kuchapisha taarifa nzito ambayo inahusishwa na suala ya Simba Sc kutinga katika hatua ya fainali ya kombe la shirikisho siku ya leo jumatano tarehe 27 Aprili.
Simba Sc wameingia fainali katika michuano hii mara baada ya kuwaondoa wababe wa soka kutoka nchini Afrika Kusini klabu ya Stellenbosch Fc kwa matokeo ya jumla ya goli moja kwa sifuri mara baada kutoka sare ya bila kufungana kwenye mchezo ambao umepigwa siku ya leo katika dimba la Moses Mabhida uko nchini Afrika kusini.
Taarifa ya klabu ya Simba Sc kutinga katika hatua ya fainali ya michuano hiyo imemuibia afisa habari wa klabu ya Yanga Sc Alikamwe ambaye amechapisha ujumbe wa vijembe kwa watani wao wa jadi Simba Sc.
Alikamwe kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram amechapisha picha ya wachezaji wa klabu ya Yanga Sc ambao walifanikiwa kuipeleka timu hiyo katika hatua ya fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika mwaka 2023.
Katika picha hiyo, Alikamwe ameambatanisha na ujumbe mzito unaoeleza kwamba hiki walichokifanya Simba Sc kwa kuingia katika hatua ya fainali ya michuano hakina maajabu wala sio jambo jipya kwa sababu Yanga Sc aalifanya hivyo mnamo mwaka 2023.
A Student Made a Discovery About Joints in Tanzania, United Republic Of
A Method that Can be Used at Home
Pillsen
by TaboolaSponsored Links
Alikamwe ameeleza wazi kwamba Simba Sc wamefanya kitu ambacho kimewahi kufanywa na Yanga Sc miaka kadhaa iliyopita hivyo hawana sababu ya kuendelea kushangilia na kupiga kelele nyingi mpaka pale watakaposhinda taji hilo mbele ya mpinzani wao ajaye.
Kwa taarifa hii iliyotolewa na Alikamwe ni wazi kwamba atakuwa anawaombea njaa Simba Sc kwamba wasishinde mechi zao fainali ambazo watacheza dhidi mshindi atakayepatikana kwenye mechi nyingine ambayo itawakutanisha CS Constantine na RS Berkane.
Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa
app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii




No comments