Subscribe Us

Breaking News

Mchakato wa kuchagua Papa mpya wa Kanisa Katoliki kuanza Mei, 7


Makadinali wa Kanisa Katoliki

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Baraza la Makadinali wa Kanisa Katoliki linalofahamika kama ''conclave'' linatarajiwa kuanza kikao chake cha siri cha kumchagua kiongozi mpya wa kanisa hilo kuanzia tarehe 7 mwezi Mei, kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Vatican siku ya Jumatatu.

Uamuzi wa kuanza kwa mchakato huo uliafikiwa katika kikao cha faragha cha makadinali kilichofanyika Vatican, kikao cha kwanza tangu mazishi ya Papa Francis yaliyofanyika Jumamosi.

Jumla ya makadinali 135 kutoka mataifa mbalimbali, wote wakiwa na umri wa chini ya miaka 80, wanastahiki kushiriki katika mchakato huo wa kumpata Papa mpya wa Kanisa lenye waumini wapatao bilioni 1.4 duniani kote.

Ukumbi wa Sistine Chapel, wa karne ya 16 na ambao ndio hufanyika kongamano hilo lenye usiri, ulifungwa kwa watalii siku ya Jumatatu ili kuruhusu maandalizi ya kura hiyo muhimu.

Katika historia ya hivi karibuni, mikutano miwili za awali mwaka 2005 na 2013 zilidumu kwa siku mbili pekee.

Hata hivyo, Kadinali Anders Arborelius wa Sweden amesema kikao kijacho huenda kikachukua muda mrefu zaidi, kwa kuwa makadinali wengi walioteuliwa na Papa Francis hawajawahi kukutana ana kwa ana.

Papa Francis, ambaye aliongoza Kanisa hilo kuanzia mwaka 2013 hadi kifo chake Aprili 21 akiwa na umri wa miaka 88, alijitahidi kulifanya Kanisa kuwa jumuishi zaidi kwa kuwateua makadinali kutoka maeneo ambayo awali hayakuwa na wawakilishi, kama vile Myanmar, Haiti na Rwanda.

“Hatujafahamiana,” alisema Kadinali Arborelius, akionyesha changamoto ya kufikia mwafaka miongoni mwa makadinali.

Vatican ilibainisha kuwa tarehe ya mapema zaidi kwa kuanza uchaguzi huo wa siri ilikuwa Mei 6, lakini kuanza Mei 7 kutawapa makadinali muda zaidi wa majadiliano ya jumla kabla ya kuingia kwenye shughuli ya kupiga kura.

Kwa wastani, chaguzi kumi zilizopita zilichukua siku tatu kufikia uamuzi wa mwisho.

Mazishi ya Papa Francis yalifanyika Jumamosi na yalihudhuriwa na umati uliokadiriwa kufikia watu 400,000 waliomiminika kushuhudia maandamano ya kuelekea eneo lake la mazishi katika Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu.

Kadinali Walter Kasper wa Ujerumani aliambia gazeti la La Repubblica kwamba wingi wa waombolezaji ni ishara ya hamu ya Wakatoliki wengi kuona uongozi unaoendeleza mwelekeo wa mageuzi ulioanzishwa na Francis.

Akiwa Papa wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini, Francis alifungua milango ya mijadala kuhusu masuala yenye utata, kama vile uwezekano wa kuwapa wanawake daraja takatifu na kujumuisha vema Wakatoliki wa LGBTQ.

Pia unaweza kusoma:



Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa

                               app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii 

No comments