Subscribe Us

Breaking News

MZIZE APEWE ULINZI, KASI YAKE INAFURAHISHA

KASI ya mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize ambaye ni mzawa kwenye eneo la ushambuliaji inafurahisha kutokana na kuzidi kuwa bora kila anapokuwa ndani ya uwanja hivyo inabidi aongezewe ulinzi na waamuzi akiwa ndani ya uwanja asiumizwe kwa makusudi.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo dhidi ya Tabora United uliochezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi alikuwa ni miongoni mwa wachezaji ambao walichezewa faulo ndani ya uwanja jambo ambalo linaongeza hatari kwa mchezaji kuwa nje ya uwanja na kutokuwa fiti ni adui namba moja kwa wachezaji.

Ni mabao 11 katupia ndani ya msimu wa 2024/25 wakati ubao wa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ukisoma Tabora United 0-3 Yanga, Aprili 2 2025 na yeye alitupia bao moja, bao lingine ni mali ya Prince Dube ambaye naye kafikisha mabao 11 huku lilela ufunguzi likifungwa na Israel Mwenda.

Mzize kwenye chati ya wafungaji wenye mabao mengi ni yeye peke yake anapeperusha bendera ya Tanzania ikiwa inamaanisha kwamba wazawa kwenye eneo la utupiaji kuna tatizo kubwa kwa kuwa William Edger ambaye yupo ndani ya Fountain Gate kasi yake imeonekana kuwa yakusuasua tofauti na Mzize ambaye amekuwa kwenye mwendelezo wakufunga.

Yanga ni namba moja kwenye ligi ikiwa na pointi 61 baada ya kucheza mechi 23 ambazo ni dakika 2,070 ina wastani wakuwa na hatari kila baada ya dakika 33  ndani ya uwanja ni mabingwa watetezi wa ligi. Mchezo ujao kwa Yanga ni dhidi ya Coastal Union unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC, Complex, Aprili 7 2025 saa 10:00 jioni.



Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa

                               app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii 

No comments