Uingereza itaanza kuwahasi wenye makosa ya uhalifu wa kigono

Serikali Uingereza itaanzisha matumizi ya dawa kemikali ya kuzuia hamu ya ngono kwa wenye makosa ya kingono, kama sehemu ya hatua za kupunguza hatari ya kurudia tena kufanya makosa hayo tena na kupunguza shinikizo kwenye mfumo wa magereza, ambao unaishiwa na nafasi.
Katika taarifa kwa Bunge Alhamisi kufuatia kutolewa kwa mapitio huru ya hukumu, Waziri wa sheria wa Uingereza Shabana Mahmood alisema kile kinachojulikana kama kuhasiwa kwa kemikali kitatumika katika magereza 20 katika mikoa miwili na kwamba anafikiria kuifanya kuwa kitendo cha lazima.
Hatua ya kuhasi kwa kutumia kemikali huhusisha matumizi ya dawa maalum pamoja na tiba ya magonjwa ya akili, na hulenga wahalifu wa kosa la kingono ambao wana matatizo ya kimawazo na hamu kubwa kuhusu ngono au masuala ya ngono.
"Kwa kweli, ni muhimu kwamba mbinu hii ichukuliwe sambamba na mbinu za kisaikolojia ambazo zinalenga sababu nyingine za kuudhi, kama vilekuzuwia na udhibiti [wa ngongo]," alisema.
Ingawa hakiki ilionyesha matibabu hayatakuwa muhimu kwa baadhi ya wenye makosa ya kingono kama vile wabakaji wanaofanya vitendo hivyo kwa lengo la mamlaka na udhibiti, badala ya ngono kama tendo la kujifurahisha , Mahmood alisema tafiti zinaonyesha kuwa kuhasiwa kwa kemikali kunaweza kusababisha kupunguza uwezekano wa mtu kurudia kosa hilo kwa 60%.
"Ni muhimu kwa mbinu hii kutekelezwa pamoja na hatua za kisaikolojia ambazo zinalenga kutibu sababu zingine za kosa la kingono, kama vile mtu kutaka kumdhibiti mwingine au kuwa na nguvu zaidi yake," alisema Mahmud.
Kuhasiwa kwa lengo la kudhibiti uhalifu wa kingono hufanyika pia nchini Ujerumani na Denmark kwa hiari, na nchini Poland kama lazima. google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii


No comments