AZIZ KI KURUDI YANGA SC, MAMBO MAGUMU

IKIWA upepo utakuwa mgumu kwa kiungo mshambuliaji wa Wydad, Aziz KI kwenye changamoto yake mpya huenda akarejea ndani ya kikosi cha Yanga SC ambacho kilitwaa ubingwa msimu wa 2024/25 kikiwa na pointi 82 kibindoni.
Msimu wa 2024/25 akiwa na uzi wa Klabu ya Yanga SC, Aziz Ki alikuwa ni chaguo la kwanza katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC.
Alicheza jumla ya mechi 25 akikosekana katika mechi tano pekee kati ya 30 na alifunga mabao 9 akitoa pasi 7 za mabao.
Alihusika katika mabao 16 kati ya 83 yaliyofungwa na Yanga SC iliyotwaa ubingwa wa ligi ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 82.
Msimu wa 2023/24 alikuwa MVP, kiungo bora na mfungajo bora. Alifunga mabao 21 na kutoa pasi 8 za mabao na Yanga SC ilitwaa ubingwa wa ligi. Alihusika katika mabao 29 kati ya 71 yaliyofungwa na Yanga SC.
Kwa sasa yupo ndani ya Wydad Casablanca kwa changamoto mpya chini ya Kocha Mkuu, Mohamed Benhachem ambaye inaelezwa kuwa bado hajaridhishwa na kiwango cha nyota huyo.
Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa
app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii



No comments