KHADIM ATAJWA KUIBUKIA SIMBA SC NI BEKI WA MPIRA

WAKATI beki Mohamed Hussen Zimbwe Jr ambaye amedumu Msimbazi kwa miaka 11 akitajwa kuibukia ndani ya kikosi cha Yanga SC, inaelezwa kuwa kuna beki wa kazi anakuja kumalizana na Simba SC.
Chini ya Fadlu Davids, msimu wa 2024/25, Zimbwe Jr alicheza mechi 27 za ligi na alifunga bao moja ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union ya Tanga uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.
Katika mchezo huo Simba SC iligawana pointi mojamoja na Coastal Union kwa ubao kusoma Simba SC 2-2 Coastal Union.
Taarifa zinaeleza kuwa Khadim Diaw ambaye ni beki wa kushoto huenda akasaini dili ndani ya kikosi cha Simba SC kuelekea msimu wa 2025/26 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Diaw anaitumikia Al Hilal ni raia wa Mauritania hivyo anakuja Bongo ndani ya Ligi Kuu Bara ya NBC ambayo ni namba nne kwa ubora.
Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa
app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii



No comments