Subscribe Us

Breaking News

YANGA SC HAITAKI UTANI YATAMBULISHA WAPYA WANNE


ISRAEL Mwenda beki wakupanda na kushuka bado atakuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Romain Folz nakufanya kuwa na wapya wanne ndani ya Julai 29 waliotangazwa Yanga SC.

Mwenda alitambulishwa Yanga SC kwenye dirisha dogo akitokea Singida Black Stars kwa mkopo kutokana na kuwa kwenye kiwango bora mabosi wa Yanga SC wamemuongezea kandarasi kuendelea kuwa Jangwani.

Kwa msimu wa 2025/26 ni uhakika atakuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi wa ligi baada ya kutwaa taji hilo msimu wa 2024/25.

Mbali na Mwenda kutambulishwa kuwa atakuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC msimu ujao kuna wengine wapya watatu waliotambulishwa Yanga SC, Julai 29 2025 ikiwa ni Tshephang Mokaila huyu ni fitnes coach.

 Mkurugenzi wa Ufundi, Paul Matthews alitambulishwa ndani ya Yanga SC Julai 29 2025 na Manu Rodriguez huyu alitambuliwa kuwa ni kocha msaidizi ndani ya Yanga SC.

Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa

                               app hii aipatikani google playstore kwa sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii 

No comments