Al Ahli Tripoli Yarudi na Mzigo: Yatupa Ofa ya Dola Milioni 2 kwa Feitoto

KLABU ya Al Ahli Tripoli ya Nchini Libya imetuma ofa nono zaidi kwenda Azam Fc kwa ajili ya kumsajili kiungo Faisal Salum ‘Feitoto’ ikiwa ni ofa ya pili baada ya ile ya awali ya Dola laki 8 kutupiliwa mbali.
Miamba hiyo ya Libya safari hii imedhamiria kumng’oa kiungo huyo wa zamani wa Young Africans Sc kunako viunga vya Azam Complex Chamazi baada ya kuwasilisha ofa ya Dola milioni 2 (takribani Tsh bilioni 4.8)
Kwa mujibu wa barua ya Al Ahli Tripoli kwenda Azam Fc iliyofichuliwa na Mwanahabari Hans Raphael, klabu hiyo ya Libya ipo tayari kulipa kitita hicho haraka iwezekanavyo ili kuinasa saini ya Feitoto huku ikiwa tayari kuweka kipengele cha Azam Fc kunufaika na asilimia 10 za mauzo ya mchezaji huyo siku za usoni.
Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa
app hii aipatikani google playstore kwa sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii


No comments