Subscribe Us

Breaking News

Karim Benzema Aibua Mjadala: “Ninaweza Kurudi Madrid”


Karim Benzema Aibua Mjadala: “Ninaweza Kurudi Madrid”

Karim Benzema ameibua tena tetesi za kurejea Real Madrid baada ya kueleza kuwa hawezi kumkatalia rais wa klabu hiyo, Florentino Perez. Akizungumza na gazeti la AS, nyota huyo wa zamani wa Madrid alisema kuwa uwezekano wa kurudi Bernabeu “upo” ilimradi Perez bado yupo madarakani.

Benzema, ambaye aliondoka Madrid mwaka 2023 na kujiunga na Al-Ittihad ya Saudi Arabia, amesema bado ana uhusiano mkubwa na klabu hiyo aliyoitumikia kwa miaka 14, akishinda mataji 25 ikiwemo Ligi ya Mabingwa mara tano. Amedai bado anaona Madrid kama “nyumba yake” na anafuatilia mechi zote.

Licha ya kuendelea kung’aa Saudi Arabia, akifunga mabao 46 katika mechi 75, mkataba wa Benzema unamalizika mwisho wa msimu huu na mustakabali wake bado haueleweki. Amedai ana ofa kadhaa kutoka Ulaya, lakini pia bado anafurahia maisha Al-Ittihad na anapanga kucheza soka kwa angalau miaka miwili zaidi.

Amesema hatafanya maamuzi ya haraka: “Lazima nichague mahali ninapojisikia vizuri. Real Madrid daima itakuwa timu yangu, lakini tutaona kitakachotokea.”


Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa

                               app hii aipatikani google playstore kwa sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii 

No comments